Habari

DKT.MWINYI AZINDUA MRADI WA KIJANA NAHODHA WA DOLA ZA KIMAREKANI MILIONI 10.6

Ahmed Hassan

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema changamoto zinazowakabili vijana ni pamoja na ukosefu wa ajira, Matumizi ya dawa za kulevya, Mimba na Ndoa za umri mdogo , Ukimwi, Afya ya akili, Ukatili na Udhalilishaji wa kijinsia yakiwemo matumizi mabaya ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).
Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo alipozindua mradi wa Kijana Nahodha wenye thamani ya dola za Kimarekani Milioni 10.6 ambao umedhaminiwa na Shirika la Misaada la Watu wa Marekani (USAID).
Mradi huu una lengo la kuwawezesha na kuwapa ujuzi vijana katika sekta mbalimbali ikiwemo Ujasiriamali wa kilimo, Ufugaji, Utalii, Uchumi wa Buluu, Stadi za Maisha na afya kwa vijana. Vile vile mradi huu umelenga kuwafikia Vijana 15,000 wenye umri kati ya miaka 15 – 25 Unguja na Pemba.
Dkt.Mwinyi amesema mradi huu wa vijana ni miongoni mwa vielelezo vya kuwepo kwa ushirikiano wa dhati kati ya Marekani na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Back to top button