Vijana Na Michezo

Uwanja wa Kimataifa wa Kairo

Ni uwanja wa rasmi ya timu ya soka ya Misri.

Uwanja huo ulianzishwa mwaka 1958 katika zama za Rais wa Misri,  Gamal Abdel Nasser, kwa jina la uwanja wa Nasser.
Uwanja huo ulishuhudia Kombe la Kimataifa la Afrika  miaka  2006 na 2019, ambapo Misri ilishinda kombe hili , pia Michuano ya Kombe la Dunia Chini ya Miaka 20 ilifanyika uwanjani humo katika mwaka 2009, uwanja huu unaweza kukusanya hadi watazamaji 75,000.
Uwanja wa Kimataifa wa Kairo ni  uwanja wa kwanza wa aina yake na uwanja wa Olimpiki katika Mashariki ya Kati na Afrika ambao uko katika  Mji wa Nasr (Nasr City) , kaskazini mashariki mwa kairo.
Uliundwa na mhandisi wa Ujerumani Werner Mars, mhandisi huyo ndiye aliyeunda Uwanja wa Olimpiki huko Berlin. Ulikamilishwa mwaka wa 1960, ulifunguliwa na Rais marehemu Gamal Abdel Nasser katika sherehe ya Mapinduzi ya Julai mwaka huo huo.
Mwaka wa 2005, uwanja wa Kairo umerekebeshwa ili ufanane na Uwanja wa Olimpiki mpya katika karne ya 21, ambapo ulikuwa mwaka wa Kombe la Kimataifa la Afrika ya 2006. Uwanja huo uko  mbali na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa kairo kwa masafa ya kilomita 10 na kilomita 30 kutoka  Katikati ya mji wa Kairo.
  • Miongoni mwa marekebesho ya uwanja kuna majengo kadha yanayoanzishwa kama mji wa michezo; kwa mtiririko huo:
  • kambi wa beseni.
  • Jumba yaliyofunikwa.
  • Uwanja wa  Mafunzo (mpira wa mikono – Mpira wa kikapu – voliboli – tenisi – Mpira wa vinyoya ).
  • Uwanja wa Hoki.
  • Uwanja wa farasi : Unahusisha Shirikisho la Kimataifa la farasi – eneo la gorofa la mita za mraba 15942 ardhi  ya michezo ni mita za mraba 73 x 138.
  • Jumba ya boga : jumba inajumuisha uwanja wa michezo kuu na (uwanja nne)  kwa mafunzo .
  • Viwanja vya michezo vya mpira wa miguu: Viwanja nne vya soka
  • Ukumbi wa wazi : vifaa vya kupokea mikutano, sherehe na maonyesho ya michezo, ulizinduliwa tarehe 14 Novemba 1984 na Rais Mohamed Hosni Mubarak juu ya eneo la 76552 m2.
Back to top button