Habari
Rais Samia Suluhu Hassan afanya mazungumzo na Moses Kuria, Waziri wa Uwekezaji, Biashara na Viwanda wa Kenya
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Waziri wa Uwekezaji, Biashara na Viwanda wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Moses Kuria, ambae pia ni Mjumbe Maalum wa Rais wa Kenya Mhe. William Samoel Ruto, mara baada ya kumkabidhi Ujumbe kutoka kwa Rais Ruto Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 03 Febuari, 2023.
Ujumbe huo ulilenga zaidi kwenye kuongeza na kudumisha undugu na pia ushirikiano wa Kiuchumi na Kibiashara.