Habari

“Mheshimiwa Rais Abdel Fattah El-Sisi akutana na Waziri wa Mambo ya Nje Wa India”

Ali Mahmoud

Mheshimiwa Rais Abdel Fattah El-Sisi leo, katika Ikulu ya India jijini New Delhi, amekutana na Mheshimiwa Subramaniam Jaishankar, Waziri wa Mambo ya Nje wa India.

Msemaji rasmi wa urais wa Jamhuri alisema kuwa Mheshimiwa Rais alisisitiza uangalifu wa Misri wa kuimarisha na kuongeza zaidi ushirikiano wa kimkakati wa muda mrefu na India, unaowakilisha nguzo muhimu kwa kudumisha usalama na utulivu katika eneo la Mashariki ya Kati, akielezea katika mfumo huu matarajio ya kuongeza uratibu na mashauriano na upande wa India kupitia kipindi kijacho kuhusu masuala mbalimbali ya kisiasa, kiusalama na kiuchumi yenye maslahi ya pamoja.

Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa India alikaribisha ziara ya Mheshimiwa Rais kwa New Delhi, akisisitiza kuwa itachangia kuunga mkono mwenendo wa mahusiano kati ya nchi hizo mbili kwa njia inayojenga na chanya, haswa kwa kuzingatia dhamira ya Serikali ya India kuimarisha mifumo ya ushirikiano wa pamoja na Misri katika nyanja mbalimbali, haswa katika ngazi ya uchumi na uwekezaji, na pia ushirikiano wa usalama na wa kijeshi.

Back to top button