Kwa mara ya Kwanza katika historia yake, Mauzo ya nje ya kilimo ya Misri yafikia tani milioni 6.5
Ali Mahmoud

Al-Sayed el-Quseir, Waziri wa Kilimo na kufufua ardhi, alitangaza ripoti ya mwisho ya mauzo ya nje ya kilimo ya Misri, ndani ya mwaka wa 2022, ambayo kwa mara ya kwanza katika historia yake ilifikia karibu tani milioni 6.5 kwa karibu dola bilioni 3.3 na ongezeko la tani elfu 800 zaidi ya mwaka uliopita, akiashiria kuwa matunda ya machungwa yanachukua nafasi ya kwanza, viazi, kisha vitunguu na maharage.
Hiyo ilikuja kulingana na ripoti iliyopokelewa kutoka kwa Dkt. Ahmed Al-Attar, Mkuu wa Usimamizi mkuu wa Karantini ya Kilimo, kuhusu jumla ya mauzo ya kilimo katika kipindi cha kuanzia Januari mosi, 2022 hadi Desemba 31, 2022, ambayo ilifikia kuhusu milioni 6, 432, 565 tani za bidhaa za kilimo, kwa ongezeko la tani 792,421 zaidi ya mwaka uliopita, ambayo ilifikia kuhusu milioni 5, 640, 144 katika kipindi hicho hicho mwaka uliopita.
Ripoti hiyo ilionesha kuwa mauzo muhimu zaidi ya kilimo ni matunda ya machungwa, viazi, vitunguu freshi, zabibu, nyanya freshi, viazi vitamu, Jordgubbar, maharage freshi, mapera, vitunguu saumu, maembe, tikiti maji, komamanga.
Al-Sayed el-Quseir, Waziri wa Kilimo na kufufua ardhi aliwashukuru maafisa wa karantini ya kilimo ya Misri, wakulima na wauzaji nje wa Misri, Baraza la Mauzo ya mazao ya kilimo, ofisi za wawakilishi wa biashara na Balozi za Misri nje ya nchi kwa juhudi zao katika kufungua masoko mapya kwa ajili ya Mazao ya kilimo ya Misri nje ya nchi, na ufuatiliaji wao wa mara kwa mara kuhakikisha matumizi ya viwango vya kimataifa ya afya ya mimea, na udhibiti mkali wa mazao ya kilimo kwa maslahi ya mauzo ya nje ya kilimo, na kusababisha ongezeko lao.