Habari Tofauti

Uzinduzi wa shughuli za Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu

Ali Mahmoud

0:00

Shughuli za mashindano ya kimataifa ya 29 ya Qur’ani Tukufu, yanayofanyika poaj na Ufadhili wa Mheshimiwa Rais Abdel Fattah El-Sisi, yalizinduliwa, Jana, katika moja ya hoteli za Kairo.

Sheikh Mahmoud Al-Khosht alifungua mashindano hayo kwa kusoma aya kutoka Qur’ani Tukufu, kwa mahudhurio ya watangazaji katika vyombo vya habari, wanasiasa na wabunge.

Wanaoshiriki katika Mashindano hayo yanayofanyika kwa muda wa siku tano, washindani 108 kutoka nchi 58 Duniani kote, wakiwemo waafrika 33, na wasuluhishi saba kutoka nchi za 7 nazo ni “Misri, Chad, Jordan, Palestina, Saudi Arabia, Sudan na Oman, kwa jumla ya tuzo za Paundi milioni 2 kulingana na maagizo ya Rais Abdel Fattah El-Sisi.

 

Wanaohudhuria shughuli za Mashindano hayo pia, ni Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, Alaa Fouad, Waziri wa Mabaraza ya Bunge, Dkt. Shawqi Allam, Mufti Mkuu wa Jamhuri, Bw. Mahmoud Al-Sharif Naqib Al-Ashraf, na Dkt. Nazir Ayyad, Katibu Mkuu Mkusanyiko wa Utafiti wa Kiislamu, kwa niaba ya Mheshimiwa Imam Mkuu Dkt. Ahmed Al-Tayeb, Sheikh wa Al-Azhar.

Back to top button
اكتب رسالتك هنا
1
تواصل معنا
اهلا بك في بوابة " مصر الآن"