Habari

RAIS DK.MWINYI AKUTANA BALOZI  WA BRAZIL

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amekutana na Balozi wa Brazil nchini Tanzania Mhe.Gustavo Martins Nogueira na ujumbe wake  Ikulu Zanzibar kwa kujitambulisha tarehe: 13 Mei 2024.

Katika mazungumzo yao wamegusia kuendeleza  uhusiano uliopo kati ya Zanzibar na Brazil katika miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo afya,  barabara, uwanja wa ndege wa Pemba, utalii, fursa za uwekezaji wa mafuta na gesi Zanzibar, na biashara hasa ya sukari.

Back to top button