Habari Tofauti

Fuateni  Sheria na taratibu za manunuzi  kwenye utekelezaji wa miradi

0:00

 

 

 

Kamati ya Kudumu ya Bunge za Serikali za Mitaa (LAAC) imeiagiza  Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti kuhakikisha inafuata sheria,kanuni na  taratibu za ununuzi kila inapoanza kutekeleza miradi ya ujenzi katika Halmashauri hiyo.

Agizo hilo limetolewa leo  Machi  23,2024 na  Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa Mheshimiwa Staslaus Mabula alipokagua mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Serengeti, Mkoani Mara

Mheshimiwa Mabula amesema kazi ya ujenzi wa hospitali hiyo kimefanyika kiufundi na ustadi wa hali ya juu lakini utaratibu wa ununuzi haukufuatwa.

Amesema kuwa kwenye ujenzi wa hospitali hiyo taratibu nyingi za ununuzi zimekiukwa ikiwemo ununuzi wa vifaa vya ujenzi kukunuliwa  kwa wazabuni, wasio idhinishwa na wakala la ununuzi serikali GPSA, nukuu za bei kutoidhinishwa na Bodi ya Zabuni ya Halmashauri

Kamati imeiagiza Halmashauri kuhakikisha  inajibu hoja 10 za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka 2021/22 na kuhakikisha wanawasilisha vielelezo muhimu vinazohitajika ili kufunga hoja hizo.

Aidha Kamati imemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kuhakikisha anasimamia ukusanyaji wa Mapato na kuhakikisha fedha hizo zinapelekwa benki kwa kuwa bila kufanya hivyo ni kukiuka utaratibu wa fedha za Serikali hivyo haitosita kuielekeza Serikali kuwachukuli hatua  watumishi wanaokiuka utaratibu wa ukusanyaji wa mapato.

Back to top button
اكتب رسالتك هنا
1
تواصل معنا
اهلا بك في بوابة " مصر الآن"