Habari Tofauti

Soko la Kariakoo kukamilika Oktoba Ijayo

0:00

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amesema ujenzi wa soko la Kariakoo inatarajiwa kukamilika Oktoba 2023.

Mradi huo ulianza kutekelezwa Januari mwaka 2022 na ujenzi wake ulitokana na kuungua moto kwa soko hilo.

Makalla ameyasema hayo jijini Dar es Salaam leo, Februari 5, 2023 alipohotubia katika maadhimisho ya miaka 46 ya kuzaliwa kwa CCM.

Amebainisha ujenzi wa soko hilo utakapokamilika wafanyabiashara 3,500 wataingia ukilinganisha na 1,200 waliokuwepo awali.

“Wahanga wa ajali ya moto iliyotokea mwaka juzi ndiyo watakaopewa kipaumbele, kisha wengine wataruhusiwa kuingia,” amesema RC Makalla.

Hata hivyo, amesema litakapokamilika biashara zitafanyika kwa saa 24 ndani ya soko hilo.

Katika hatua nyingine, Makalla amebainisha kupitia mradi wa uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam awamu ya pili (DMDP II) daraja litakalounganisha eneo la Magomeni hadi Fire litajengwa.

“Hata wale wenzetu wa pale Jangwani (Yanga) patabadilika hapatakuwa kama ilivyo sasa,” amesema.

Back to top button
اكتب رسالتك هنا
1
تواصل معنا
اهلا بك في بوابة " مصر الآن"