Uchumi

MISRI YAAHIDI KUSHIRIKIANA NA TANZANIA KUIMARISHA SEKTA YA MIFUGO NA UVUVI

0:00

 

Tarehe 07 Februari, 2024 Mhe. Mej. Jen. Richard Mutayoba Makanzo, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Misri alifanya mazungumzo na Profesa Saad Mousa, Msimamizi wa Mahusiano Kutoka Wizara ya Kilimo na Mamlaka ya Kusimamia Marufuku ya Mimea ili kuimarisha uhusiano na ushirikiano pamoja na kuangalia maeneo mapya ya ushirikiano baina ya Wizara ya Kilimo ya Tanzania na Wizara ya Kilimo ya Misri.

Profesa Saad alisisitiza haja ya kuhuisha na kutekeleza kikamilifu Makubaliano ya Ushirikiano (MoU) iliyotiwa saini mwaka 2018 katika sekta ya kilimo kupitia Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC).

Pia, alieleza haja ya kuhuisha MoU 2 katika sekta ya Kilimo zilizotiwa saini ili kuongeza wigo wa mashirikiano katika sekta ya mifugo, vifaa vya kilimo, umwagiliaji maji, uvuvi na mafunzo ya aina mbali mbali kutoa fursa ya Maafisa wa kilimo kutoka Tanzania, Bara na Zanzibar kunufaika na fursa hizo.

Alieleza kuwa Jumla ya Wanafunzi 10 hadi 15 hupata mafunzo ya kozi fupi nchini Misri kila mwaka katika sekta ya Kilimo na Uvuvi.

Aidha, alieleza mafunzo yanayotolewa na wataalamu wa Kilimo kutoka Misri huko Zanzibar kupitia shamba la pamoja liloanzishwa mwaka 2003.

Naye Mhe. Mej. Jen. Richard M. Makanzo alitoa shukuran kwa mashirikiano mazuri yaliopo baina Tanzania na Misri katila sekta mbali mbali ikiwa ni pamoja na Kilimo.

Alisisitiza haja ya kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano uliopo kwa kuimarisha sekta ya uvuvi, ufugaji wa Samaki na kilimo cha mazao mbali mbali kwa uwekezaji wa Viwanda na mashamba makubwa kuunga mkono Juhudi za Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia mradi ‘ ‘Building a Better  Tomorrow Initiatives’ ili kujenga fursa nyingi zaidi za ajira kwa vijana.

Alizungimzia mazingira mazuri ya uwekezaji yaliopo Tanzania, ardhi nzuri ya kilimo, vyanzo mbali mbali vya maji kwa kilimo cha umwagiliaji, pamoja na rasilimali za madini, vivutio vya utalii kama mbuga za wanyama, mlima Kilimanjaro na fukwe nzuri za bahari ya Hindi katika visiwa vya Zanzibar ili kuvutia Wawekezaji.

Pia uwepo wa mifugo mingi Tanzania ni miongoni mwa fursa ambayo Misri inaweza kuitumia kikamilifu katika kuimarisha biashara baina ya Misri na Tanzania..

Back to top button
اكتب رسالتك هنا
1
تواصل معنا
اهلا بك في بوابة " مصر الآن"