Uchumi

Kwa mara ya Kwanza kabisa / Misri yashiriki kwenye BRICS kama mwanachama kamili na yatoa wito wa kuimarisha ushirikiano na uratibu kati ya nchi za BRICS

0:00

 

Misri ilishiriki kwa mara ya kwanza katika mikutano ya BRICS baada ya kujiunga kama mwanachama kamili kuanzia Januari 2024, ambapo Balozi Rajy El-Etreby, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Uhusiano wa Kiuchumi wa pande nyingi na mwakilishi wa Misri katika BRICS, alishiriki katika mikutano ya wawakilishi binafsi wa viongozi wa BRICS, iliyofanyika Moscow mwishoni mwa Januari, kwa mahudhurio ya Balozi Nazih El-Nagary, Balozi wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri huko Moscow.

Balozi El-Etreby alisema kuwa mkutano huu ni wa kwanza katika mfululizo wa mikutano na matukio yaliyoandaliwa na urais wa Urusi wa BRICS wakati wa mwaka huu kujadili ushirikiano katika nyanja mbalimbali, na pia inakuja baada ya nchi waanzilishi wa mkutano huo kuzialika nchi kadhaa kujiunga na wanachama wa kundi hilo, ikiwa ni pamoja na Misri, Falme za Kiarabu, Iran na Ethiopia, akisisitiza kuwa uanachama wa Misri katika mkutano huo unaendana na uzito wake wa kimkakati katika ngazi mbalimbali, na michango yake kwenye kukuza amani na maendeleo kwenye ngazi za kikanda na kimataifa, pamoja na fursa nyingi zinazotolewa na uchumi wa Misri ili kuvutia uwekezaji kutoka nchi za BRICS na kuongeza kubadilishana biashara nao, vipaumbele vya Misri kuelekea BRICS ni pamoja na kuendeleza juhudi za mabadiliko ya viwanda, na kuimarisha ushirikiano kwenye nyanja za nishati, usalama wa chakula, uhamishaji wa teknolojia na vifaa.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje pia alieleza kuwa mkutano huo ulishuhudia mapitio ya urais wa Urusi wa BRICS juu ya vipengele vikuu vya mpango wa utekelezaji ulioandaliwa kwa mwaka huu, na kuelekea mkutano wa kumi na sita wa BRICS utakaofanyika Oktoba 2024 kwenye mji wa Kazan nchini Urusi, na kwamba nchi wanachama ziliwasilisha maono yao kuhusu vipaumbele vinavyopaswa kuzingatia katika kipindi kijacho.

Katika suala hilo, alisema kuwa maono na mapendekezo ya Misri kuhusu kuimarisha ushirikiano na uratibu kati ya nchi za BRICS yamepata msaada mkubwa, ikiwa ni pamoja na kusaidia mifumo ya uratibu kuhusu kurekebisha mfumo wa uchumi wa kimataifa, kusukuma juhudi za kuongeza uwakilishi wa nchi zinazoendelea katika mifumo ya kifedha ya kimataifa na fedha ili kuonesha uzito wao wa kiuchumi, pamoja na kuimarisha mahusiano kati ya BRICS na Bara la Afrika, kuanzisha mahusiano ya kitaasisi kati ya mamlaka ya uwekezaji ya BRICS, na kufanya kazi ya kuendeleza mifumo ya malipo kati ya nchi za BRICS kwa sarafu za kitaifa.

Back to top button
اكتب رسالتك هنا
1
تواصل معنا
اهلا بك في بوابة " مصر الآن"