Uchumi

BANDARI MPYA  YA ABIRIA KUJENGWA ZANZIBAR

0:00

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema ujenzi wa  bandari mpya ya abiria eneo la Mpiga Duri ni azma ya Serikali  kuondoa msongamano katika bandari ya Malindi sehemu ya abiria ambayo ina changamoto ya nafasi.

Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo katika hafla ya  utiaji saini mkataba wa ushirikiano kati ya Serikali na kampuni ya ZF DEVCO ya ujenzi wa bandari ya abiria eneo la Mpiga Duri, Ikulu Zanzibar tarehe 09 Januari 2024.

Aidha Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa bandari hiyo ya kisasa itakuwa na eneo la boti za abiria, usafiri wa boti za mizigo, taxi za baharini, maduka ya kisasa, ndege zinazotua na kuruka baharini, kituo cha umma cha mabasi, hoteli ya nyota tano, ukumbi wa kimataifa wa mikutano pamoja na eneo  la maegesho ya boti.

Vilevile gharama za mradi wa ujenzi huo ni dola za kimarekani milioni 400 , na utakamilika kwa miezi 36 ijayo.

Hafla hiyo imehudhuriwa na Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania Mhe. Wiebe De Boer, Viongozi mbalimbali wa Serikali na Vyama vya siasa.

Back to top button
اكتب رسالتك هنا
1
تواصل معنا
اهلا بك في بوابة " مصر الآن"