Uchumi

Balozi wa Tanzania akutana na Uongozi wa El Sewedy Electric

0:00

Mej. Gen. Richard Mutayoba Makanzo, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania siku ya tarehe 04 Januari, 2024 ameonana na uongozi wa El-Sewedy Electric, chini ya uongozi wa Eng. Ahmed El Sewedy, Mwenyekiti na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo katika Makao Makuu ya Kampuni hiyo, New Cairo nchini Misri.

Mhe. Balozi alizungumzia haja ya kuendeleza uhusiano mzuri uliopo baina ya Tanzania na Misri na kuimarisha ushirikiano kwa uendelezaji miradi mikubwa katika sekta mbali mbali kama ujenzi, kilimo, na uwekezaji katika viwanda vya usindikaji matunda, vifaa vya ujenzi, umeme na kadhalika.

Aidha, aliipongeza Kampuni hiyo kwa utekelezaji mzuri wa ujenzi la Ujenzi wa Bwawa la Mw. J. K. Nyerere huko Rufiji, mradi unaoweka alama muhimu ya ushirikiano baina ya Tanzania na Misri.

Aidha, mradi huo unaidhibitishia dunia kwamba matatizo ya Afrika yanaweza kutatuliwa na Waafrika wenyewe kutokana na uwezo, utaalamu na utayari wa kuliendeleza Bara la Afrika.

Nae Eng. Ahmed El-Sewedy, alimpongeza Balozi Mej. Gen. Richard M. Makanzo kwa kuteuliwa kwake kuiwakilisha Tanzania na nchi nyengine 6, jukumu ni kubwa na kumkaribisha nchini Misri.

Eng. Ahmed El-Sewedy, alimthibitishia Balozi Makanzo kwamba Kampuni yake iko tayari kufanya uzinduzi wa Bwawa muda wowote kutegemea ratiba ya Mhe. Dr. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Vilevile, Kampuni iko tayari kuwekeza Tanzania miradi mikubwa na pia itashirikiana na Ubalozi Bega kwa Bega kurahisisha utekelezaji wa majukumu yake nchini Misri.

Aidha, Eng. Ahmed El-Sewedy amesema tayari mradi wa kiwanda cha uzalishaji vifaa vya umeme Kigamboni – Dar Es Salaam kimeanza uzalishaji na bidhaa zinauzwa nchi mbali mbali ikiwa ni pamoja na Kenya, D.R. Congo, n.k.

Pia Kampuni inaazisha Industrials Park kubwa huko Kibaha ambapo Makampuni makubwa ya uzalishaji dawa za binaadamu, vifaa vya ujenzi, mbolea na kadhalika kutoka Misri yameonyesha utayari kuwekeza hapo.

Sambamba na hayo, Kampuni ya El -Sewedy inakusudia kuanzisha miradi mikubwa ya uzalishaji mazao mbali mbali katika sekta ya kilimo ambapo juhudi za kutafuta eneo la ardhi kwa mradi huo zinaendelea.

Back to top button
اكتب رسالتك هنا
1
تواصل معنا
اهلا بك في بوابة " مصر الآن"