Habari

Mwanzo wa Uanachama wa Misri kwenye Baraza la Amani na Usalama la Afrika

 

Uanachama wa Misri kwenye Baraza la Amani na Usalama la Afrika kwa kipindi cha kuanzia Aprili 2024 hadi Machi 2026 ulianza mapema Aprili, baada ya Misri kuchaguliwa kwa kauli moja wakati wa mikutano ya kilele ya Umoja wa Afrika mnamo Februari 2024, kama mwakilishi wa kanda ya Afrika Kaskazini, inayoonesha shukrani na imani ya nchi za kindugu za kanda ya Kaskazini mwa Afrika, pamoja na nchi zote za bara, kwa juhudi na kujitolea kwa Misri katika kukuza amani, usalama na utulivu Barani Afrika.

Baraza la Amani na Usalama limefanya mkutano wake wa kwanza na muundo mpya wa Baraza hilo, uliojumuisha sehemu ya sherehe kwa nchi wanachama wapya kupandisha bendera za nchi zao katika makao makuu ya Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika, ikifuatiwa na kikao cha kushughulikia masuala muhimu ya Amani na usalama barani humo na kuzingatia hali ya Somalia.

Dkt. Mohamed Gad, Balozi wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri nchini Ethiopia na Mwakilishi wa Kudumu wa Umoja wa Afrika, aliwasilisha maono ya Misri ya kuimarisha Amani na Usalama Barani Afrika, akisisitiza kuwa changamoto za usalama zinazoshuhudiwa na bara hilo zinahitaji ushiriki mkubwa kutoka kwa Tume ya Umoja wa Afrika kwa ajili ya kudumisha Amani na Usalama wa kikanda, na kutoa wito wa maendeleo ya mbinu na utaratibu wa kazi ya Baraza ili kusaidia juhudi zinazoendelea za mageuzi ya kitaasisi, kwa njia inayoongeza ufanisi wa Baraza. Pia alisisitiza haja ya kuchukua njia kamili ya kushughulikia changamoto za usalama na maendeleo zinazolikabili bara hilo, ambalo kubwa ni vita dhidi ya ugaidi na kuenea kwa migogoro ya silaha katika nchi nyingi za bara.

Balozi Gad pia alisisitiza umuhimu wa juhudi za ujenzi na maendeleo katika kukabiliana na changamoto za amani na usalama Barani Afrika kuhusiana na uongozi wa Misri katika faili ya kufufua na kuimarisha sera ya Umoja wa Afrika kwa ajili ya ujenzi na maendeleo baada ya mgogoro, na Cairo mwenyeji wa makao makuu ya Kituo cha Umoja wa Afrika cha Ujenzi na Maendeleo ya Baada ya Mgogoro, akisisitiza haja ya juhudi za pamoja za kumaliza migogoro katika nchi za bara, haswa katika nchi jirani, ili kusaidia kuimarisha amani na usalama wa kikanda. Alibainisha umuhimu wa kutanguliza uhusiano kati ya amani, usalama na maendeleo, pamoja na uhusiano kati ya mabadiliko ya hali ya hewa, amani na usalama, ili kusaidia kufikia malengo ya Ajenda ya Maendeleo ya Umoja wa Afrika 2063.

Back to top button