Habari

RAIS DK.MWINYI AWAAPISHA VIONGOZI  WA TUME YA UCHAGUZI ZANZIBAR

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amemwapisha Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Mheshimiwa Jaji George Joseph Kazi na wajumbe wake sita wakiwemo Mhe.Jaji Aziza Iddi Suwedi, Idrisa Haji Jecha, Juma Haji Ussi, Halima Mohamed Said, Ayoub Bakar Hamad, na Awadh Ali Said iliyofanyika Ikulu Zanzibar  leo tarehe 28 Agosti 2023.

Viongozi mbalimbali wa Serikali, vyama vya siasa , Wakuu wa Vyombo vya ulinzi na Usalama, viongozi  wa dini wamehudhuria hafla hiyo fupi.

Back to top button