Siasa

Rais El-Sisi ampokea Mkurugenzi wa CIA William Burns

Mervet Sakr

“Rais Abdel Fattah El-Sisi alipokea Jumatatu Bw. William Burns, Mkurugenzi wa Shirika la Ujasusi la Marekani, kwa mahudhurio ya Meja Jenerali Abbas Kamel, mkuu wa Idara Kuu ya Ujasusi.”

Msemaji rasmibwa Urais alisema kuwa Rais alimkaribisha afisa huyo wa Marekani na kuomba kufikisha salamu zake kwa Rais wa Marekani Joe Biden, akisisitiza nguvu ya mahusiano kati ya Misri na Marekani na ujali wa Misri wa kuimarisha na kukuza ushirikiano thabiti kati ya nchi hizo mbili katika nyanja mbalimbali, haswa katika ngazi za usalama na ujasusi, na kuunga mkono juhudi za kurejesha utulivu katika Mashariki ya Kati kutokana na changamoto inazozishuhudia.

Kwa upande wake, Bw. Burns aliwasilisha kwa Rais salamu za Rais Biden, pamoja na hakikisho lake juu ya umuhimu na nguvu ya mahusiano kati ya Misri na Marekani, huku Washington ikitazamia katika kipindi kijacho cha kuendeleza ushirikiano na mahusiano ya ushirikiano na Misri, ambayo ni kitovu cha mvuto wa eneo la Mashariki ya Kati na nguzo ya usalama na utulivu chini ya uongozi wa Rais, haswa katika hatua hii nyeti ambayo inashuhudia migogoro ya kimataifa na kikanda.

Msemaji huyo alifafanua kuwa mkutano huo ulijadili njia za kuimarisha ushirikiano wa kiusalama na kijasusi kati ya nchi hizo mbili, pamoja na kubadilishana mawazo kuhusu maendeleo yanayohusiana na masuala kadhaa ya kimataifa na kikanda yenye maslahi ya pamoja.

Back to top button