Habari
DK.MWINYI AMPONGEZA RAIS SAMIA KWA MAFANIKIO YA IKULU MPYA CHAMWINO
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kwa mafanikio ya ujenzi wa majengo mapya ya Ofisi ya Rais Ikulu Chamwino kuwa ni hatua za kuendeleza dhamira ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius K.Nyerere kupitia Chama cha TANU Mwaka 1973 kwa Azimio la Dodoma kuwa Makao makuu ya Serikali.
Dk.Mwinyi ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuipatia eneo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa ujenzi wa Ofisi zake na ameahidi atajenga ofisi za SMZ Dodoma .
Pia katika Ikulu mpya ya Chamwino kumetengwa ofisi ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.