Vijana Na Michezo

Waziri wa Vijana na Michezo akutana na mwakilishi wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) nchini Misri

Mervet Sakr

0:00

Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, katika makao makuu ya Wizara hiyo katika wilaya ya serikali huko Mji Mkuu Mpya wa Utawala, amekutana na Hanan Hamdan, mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) nchini Misri, kujadili kuimarisha mifumo ya ushirikiano wa pamoja baina ya pande hizo mbili mnamo kipindi kijacho.

Waziri huyo alisema: “Wizara ya Vijana na Michezo inafanya kazi ya kukuza vijana na kukuza ujuzi wao katika tawala mbalimbali, na kuwaandaa kwa ajili ya soko la ajira ili kuweza kuendana na kasi ya maendeleo, na sambamba na hilo tunajitahidi kuwaunganisha wakimbizi na vijana wa Misri kubadilishana uzoefu na tamaduni, na tuna nia ya kukidhi haki zao zote.”

Sobhy alibainisha kuwa Wizara hiyo inatekeleza mipango na matukio mengi kwa wakimbizi, ikiwa ni pamoja na “maeneo salama, na vituo vya kidijitali”, akifafanua kuwa mradi wa nafasi salama unalenga kutoa mazingira salama kwa wanawake na wasichana wanaoishi nje na kuwaunganisha katika jamii ya Misri, kwani maeneo salama hutoa shughuli mbalimbali kama vile uhamasishaji dhidi ya ukatili wa kijinsia, kuongeza uelewa wa afya ya uzazi, pamoja na mafunzo ya ufundi na uwezeshaji wa kijamii.

Dkt. Ashraf Sobhy amesisitiza haja ya kuimarisha ushirikiano na UNHCR ili mafanikio ya wakimbizi hao yaendelee kupata fursa za mafunzo yanayofanikisha uendelevu na kuwapa fursa za kazi zinazowasaidia katika maingiliano yao na jamii ya Misri.

Kwa upande wake, Hanan Hamdan, mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) nchini Misri, aliishukuru Misri na Wizara ya Vijana na Michezo kwa nia ya kuwaunganisha wakimbizi katika jamii ya Misri na kuwasaidia wakimbizi, akibainisha kuwa huo ni uzoefu mzuri wa kuwaunganisha wakimbizi na kuwajua wenzao kutoka kwa vijana wa Misri na ushirikiano kati yao, akisifu kile Wizara ya Vijana na Michezo inachotoa kwa wakimbizi.

Mkutano huo ulihudhuriwa na Manal Gamal, Mkuu wa Idara kuu ya Uwezeshaji Vijana, Meja Jenerali Abdul Rahman Shalash, Mkuu wa Idara kuu ya Masuala ya Ofisi ya Waziri, Bi. Marcelia Rodriguez Farrelly, Mkurugenzi wa Idara ya Uwajibikaji kwa Jamii, Bi Judith Chan, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Uwajibikaji, Nanis Naqouri, Mkurugenzi Mkuu wa Idara Kuu ya Mipango ya Vijana, na Gihan Rashwan, Mkurugenzi Mkuu wa Idara Kuu ya Ujasiriamali na Miradi inayoibuka.

Back to top button