Vijana Na Michezo

MASHINDANO YA AFCON2023 YATUMIKA KUHAMASISHA UPIMAJI AFYA KWA HIARI KIBITI

0:00

KATIKA kudhibiti magonjwa ya mlipuko na yasiyo ya mlipuko, Wilaya ya Kibiti imeendesha zoezi la uchunguzi wa afya na utoaji chanjo kwa wananchi wa Kibiti waliokuwa wakitazama mashindano ya AFCON 2023.

Akizungumza kwa niaba ya Naibu Waziri, Ofisi ya Rais  TAMISEMI Dkt.Festo Dugange kwenye mechi ya nusu fainali ya AFCON, Mkuu wa wilaya ya Kibiti Kanali Joseph Kolombo, amewasisitiza wananchi kuendelea kuwa na utaratibu wa kunawa mikono kwa maji tiririka kwaajili ya kijikinga na magonjwa ya mlipuko.

“Mnatakiwa kunawa maji na sabuni kupunguza kiasi kikubwa cha magonjwa ikiwemo magonjwa ya Tumbo n magonjwa mengine na tahadhari hii tuiendeleze mpaka kwenye taasisi zetu unapifika nawa mikono na unapotoka nawa mikono  pia tule chakula cha moto na hiyo ni tahadhali nyingine ya kujikinga na kipindupindu”

Zoezi la upimaji Afya kwa hiari kupitia mashindano ya AFCON2023 lilizinduliwa katika viwanja vya Mbagala Zakhem mkoani Dar Es Salaam linaloendelea katika maeneo mengine nchini kwa kipindi chote cha mashindano ya AFCON 2023,  limeratibiwa na ortamisemi  kwa kushirikiana na uniceftz na mradi wa BreakthroughAction.

Back to top button
اكتب رسالتك هنا
1
تواصل معنا
اهلا بك في بوابة " مصر الآن"