Kituo cha Kitaifa cha Tafsiri chaomboleza kifo cha Mkuu wa Watafsiri Mohamed Anany
Ali Mahmoud
Kituo cha Kitaifa cha Tafsiri, kinachoongozwa na Dkt. Karma Sami, kinaomboleza Mtafsiri Mkuu Mohamed Anany, aliyefariki Dunia Jumanne asubuhi, na katika taarifa ya Dkt. karma Sami, Mkurugenzi wa Kituo cha Kitaifa cha Tafsiri alisema : “Iconi ya tafsiri katika Ulimwengu wa Kiarabu, Dkt. Mohamed Anany, amefariki leo, baada ya safari iliyojaa kutoa, iliyokuwa hatua muhimu katika historia ya tafsiri nchini Misri na Ulimwengu wa Kiarabu, na kitabu chake maarufu “Sanaa ya Tafsiri” kitabaki chenye neema isiyosahauliwa kwa wapya kwenye sanaa ya tafsiri, ambapo yeye aliwasilisha kitabu hiki kwa mtafsiri mpya anayeanza kazi katika uwanja wa kutafsiri kwa mara ya kwanza, marehemu anazingatiwa mtafsiri aliye ni mfano mzuri na kielelezo ambapo mtafiti wa kitaaluma anapaswa kumfuata, aliendelea: “Tunamwomba Mwenyezi Mungu awape watu wake, wanafunzi wake na wapenda wake, uvumilivu na subira, kazi zake na safari yake zitaendelea na zitadumu katika uwanja wa tafsiri katika ulimwengu wa kiarabu”.
Marehemu ana kazi nyingi zilizochapishwa na Kituo cha Kitaifa cha Tafsiri, ikiwa ni pamoja na: “Shakespeare: uumbaji wa utu wa binadamu”, “Encyclopedia ya Harmoniotic”, “kutongoza haiwezekani”, “vikwazo vya kitamaduni”, “kujenga tamaduni”, “maandiko kutoka katika mashairi ya hadithi ya kimapenzi ya kiingereza”, “lugha na nguvu”, hotuba na mabadiliko ya kijamii ” na ” wafikiri wa msingi kutoka nadharia ya fasihi hadi Baada ya Marxism”.
Marehemu alipata idadi kubwa ya tuzo, ikiwa ni pamoja na “tuzo ya serikali katika fasihi”, “tuzo ya ubora katika fasihi”, “Tuzo ya Refaa Al-Tahtawi katika tafsiri” na “Tuzo ya Kimataifa ya Mfalme Abdullah katika tafsiri”.