Utamduni

Waziri wa Utamaduni akutana na ujumbe kutoka Afrika Kusini kwa kukubaliana juu ya shughuli za “Msimu wa Utamaduni wa Afrika Kusini”

Mervet Sakr

0:00

Dkt. Nevine Kilani, Waziri wa Utamaduni, amekutana na ujumbe wa Wizara ya Utamaduni na Sanaa huko Afrika Kusini, kwa kujadili mifumo ya ushirikiano wa pamoja, shughuli na matukio yatakayofanyika mnamo kipindi kijacho.

Mkutano huo ulishuhudia makubaliano ya kuandaa “Msimu wa Kwanza wa Utamaduni wa Afrika Kusini”, utakaojumuisha matukio mbalimbali kati ya maonesho ya vitabu, ufundi na kazi za mikono, na warsha za pamoja kati ya timu za Misri na Afrika Kusini katika uwanja wa sanaa za maonesho, pamoja na kufanya kongamano la biashara linalojadili jukumu la utamaduni na sanaa ndani ya mfumo wa utekelezaji wa Mkataba wa Biashara Huria wa Bara, na jukwaa la kisanii la uchoraji kwenye kuta.

Dkt. Nevine El-Kilani alisisitiza maslahi ya taifa la Misri Barani Afrika, akibainisha kuwa utamaduni ni lengo kubwa katika makubaliano na kumbukumbu nyingi za maelewano zilizohitimishwa na taifa la Misri na nchi za bara hilo.

Waziri huyo wa Utamaduni amesema msimu wa kwanza wa utamaduni wa Afrika Kusini utakaofanyika katika miezi ijayo, utadumu kwa siku kumi, na ni mlango mpya wa kujenga madaraja ya ushirikiano na Afrika Kusini, na fursa ya kuanzisha tamaduni na sanaa za kipekee na tofauti za Kiafrika.

Dkt. Iman Negm, Mkuu wa Sekta ya Mahusiano ya Utamaduni wa Kigeni, alisisitiza kuwa jukwaa hilo litachanganya sanaa tajiri za Misri na sanaa mashuhuri za Afrika Kusini, zitakazotoa fursa ya kufungua upeo mpya wa ushirikiano wa kiutamaduni na Afrika Kusini.

Negm amesema kuwa matukio hayo yataandaliwa kwa kushirikiana na sekta mbalimbali za wizara hiyo ambazo ni katika utangulizi wake wa Baraza Kuu la Utamaduni, Jumba la Opera la Kairo, Mamlaka Kuu ya Majumba ya Utamaduni na Mfuko wa Maendeleo ya Utamaduni.

Kwa upande wake, Rufus Matbe, Mkurugenzi wa Idara ya mahusiano ya kimataifa katika Wizara ya Utamaduni na Sanaa nchini Afrika Kusini, alielezea furaha yake kwa kushirikiana na Wizara ya Utamaduni ya Misri, akieleza kuwa lengo la msimu wa utamaduni wa Afrika Kusini ni kuutambulisha umma wa Misri kwa sanaa na urithi wa Afrika Kusini uliotolewa kupitia vizazi kupitia mfululizo wa shughuli zitakazoandaliwa kwa ushirikiano na Wizara ya Utamaduni ya Misri.Na Matbi alielezea kuvutiwa kwake na ukuu wa ustaarabu wa Misri, historia na urithi, na urithi na makaburi ya akiolojia aliyotembelea katika siku zilizopita ili kujua maeneo matukio yatakayofanyika.
Ujumbe wa Wizara ya Utamaduni na Sanaa ya Afrika Kusini ulijumuisha Bi Masana Shikika, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni, na Bi Melissa Magaka, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Matukio.

Back to top button
اكتب رسالتك هنا
1
تواصل معنا
اهلا بك في بوابة " مصر الآن"