HabariUtamduniVijana Na Michezo

Sobhy atembelea Banda la Wizara kwenye Maonesho ya Kitabu na Kukagua Idadi ya Shughuli katika Pembezoni mwa Maonesho hayo

Mervet Sakr

0:00

 Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo ametembelea kukagua shughuli za vijana zilizofanyika katika toleo la 54 la Maonesho ya Kimataifa ya Kitabu ya Kairo kwenye Kituo cha Maonesho cha Kimataifa cha Misri huko The Fifith Settlement.

Waziri ameanza ziara hiyo kwa kutembelea makao ya msafara wa vijana na hali ya hewa uliozinduliwa pembezoni mwa Misri kuwa mwenyeji wa Mkutano wa kilele ya Hali ya Hewa, uliopatikana katika makao ya maonesho ili kukuza ajenda ya hali ya hewa na urais wa misri kwa mkutano wa vyama vya majimbo kwa mabadiliko ya hali ya hewa, pamoja na kukagua michezo ya burudani ambayo wizara ya vijana na michezo inaitoa kwa wanaotembelea maonesho kama vijana na watoto.

Pia, waziri amekutana na idadi ya waliojitolea wa Wizara ya Vijana na Michezo ” Mimi ni Mjitolea” wanaofanya majukumu ya utaratibu wa maonesho ya kitabu kwa mwaka wa sita, na amewashukuru na kuwasifu jukumu lao tofauti.

Aidha, Waziri huyo ameshuhudia onesho la kikundi cha wasanii kutoka kwa wachipukizi wa Port Said, na kufuatiwa na ziara kwa banda la wizara, kupitia kwake amehudhuria kikao cha kukuza Mikutano ya Michezo Sports Expo, ambapo Mhandisi. Hazem Hamada, Mkurugenzi Mtendaji kwa Delta Konnex, Mtaratibu wa Matukio ya maonesho, ametangaza kukaa kwake kutoka 22 hadi 24 Februari, pamoja na Ufadhili wa Rais wa Jamhuri.

Kwa upande wake, Bi.Jihan Hanafy Mkuu wa Idara Kuu kwa Wachanga ameonesha shughuli za kifani na za kiutamaduni ambazo Wizara imezitoa kupitia maonesho hiyo, pamoja na maonesho ya Dkt. Mohammed Abdel Daim, Mkurugenzi Mtendaji wa jukwaa la Kayani kwa juhudi za jukwaa katika kukuza matukio ya vijana na michezo katika ngazi ya Jamhuri.

Pia Dkt, Ashraf Sobhy amekutana na Dkt, Nevin Al-Kilani, Waziri wa Utamaduni, Waziri alimpongeza kwa mafanikio ya maonesho hayo, tofauti na utofauti mkubwa unaoshuhudiwa na maonesho hayo.

Pembazoni mwa ziara yake, Waziri amehudhuria sherehe ya kusainiwa kwa Mwakilishi Mhandisi Ashraf Rashad, na Mwakilishi Dkt. Mahmoud Hussein, Mkuu wa Kamati ya Vijana na Michezo katika Baraza la Bunge.

Kupitia ziara hiyo, Waziri ameambatana na Jenerali Ismail Al_far, Mkuu wa Sekta ya Vijana, Jenerali Abdul Rahman Shalash, Mkuu wa Idara Kuu ya Ofisi ya Waziri, Bi. Jihan Hanafy, Mkuu wa Idara kuu ya Maendeleo ya Wachanga, Bi. Iman Osman, Mkurugenzi Mkuu wa wenye talanta, Bi. Hala Osman, Mkurugenzi Mkuu wa programu ya wachanga, na Mustafa Ezz Al-Arab, mratibu wa ushiriki wa Wizara katika maonesho hayo ya Kitabu.

Back to top button
اكتب رسالتك هنا
1
تواصل معنا
اهلا بك في بوابة " مصر الآن"