Habari Tofauti

TANZANIA: ZIARA WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII- WILAYANI LUDEWA

Victoria C Mwanziva

0:00

Wilaya ya Ludewa tulimpokea Waziri wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Balozi Dkt. Pindi Chana na kumuongoza kwenye miradi mbalimbali inayotekelezwa chini ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Wilayani Ludewa.

Mhe. Waziri alifanya ziara ya siku moja Wilayani Ludewa na kuzindua zoezi la upandaji miti zaidi ya miti 300 ilipandwa katika shule ya sekondari Ludewa na kuhamasisha upandaji miti kwa lengo la kutunzaji mazingira.

Tulimpa taarifa kuhusu zoezi la upandaji miti na kumhakikushia litakuwa endelevu kwani eneo hilo limepandwa miti mingi, kwa wiki la uzinduzi jumla ya miti 600 imepandwa na zaidi ya mizingi ya nyuki 100 imewekwa katika msitu wa eneo hilo kwa lengo la kuanzisha biashara ya asali pindi itakapo anza kurinwa.

Kwa upande wangu nilimuahidi Waziri wa Maliasili kuwa Wilaya ya Ludewa itaendelea kutoa elimu kwa vijana na watu wote ya umuhimu wa utunzaji mazingira na kuyafanya mazingira hayo kuwaingizia kipato.

Katika hatua nyingine Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana alikabidhi gari moja lenye thamani ya milioni 170 kwa Wakala wa Huduma za Misitu TFS Wilaya ya Ludewa kwa lengo la kusaidia ufuatikiaji, na utaoaji elimu kwa wananchi wa vijijini juu ya umuhimu wa utunzaji mazingara na kutochoma moto ovyo.

Mwisho alimaliza kwa kusema kuwa wizara yake itaendelea kuwa jirani na Halmashauri zote nchini kwa kutoa miti ya kutunza vyanzo vya maji, miti ya kibiashara.

 

Back to top button
اكتب رسالتك هنا
1
تواصل معنا
اهلا بك في بوابة " مصر الآن"