Habari

DK.MWINYI AMPONGEZA RAIS SAMIA KWA MAFANIKIO YA IKULU MPYA CHAMWINO

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kwa mafanikio ya ujenzi wa majengo mapya ya Ofisi ya Rais Ikulu Chamwino  kuwa ni hatua za kuendeleza dhamira ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu  Julius K.Nyerere kupitia Chama cha TANU Mwaka  1973 kwa Azimio la Dodoma kuwa Makao makuu ya Serikali.

 Dk.Mwinyi ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuipatia eneo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  kwa ujenzi wa Ofisi zake na ameahidi atajenga ofisi za SMZ  Dodoma .

Pia katika  Ikulu mpya ya Chamwino kumetengwa ofisi ya  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

زر الذهاب إلى الأعلى