Vijana Na Michezo

Waziri wa Vijana na Michezo, Mkuu wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Mikono na Mkuu wa Kamati ya Olimpiki ya Misri wajadili maelezo ya kuomba kuandaa Michezo ya Afrika ya 2027 na Michezo ya Olimpiki ya 2036

Mervet Sakr

0:00

Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alifanya mkutano na Dkt. Hassan Mustafa, Mkuu wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Mikono, na Mhandisi Hisham Hatab, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kamati ya Olimpiki ya Misri, kwa kujadili kujifunza azma ya Misri ya kuandaa Michezo ya Afrika ya 2027 na Michezo ya Olimpiki ya 2036,kwa mahudhurio ya kundi la viongozi wa Wizara ya Vijana na Michezo.

Waziri wa Vijana na Michezo alithibitisha kuwa utafiti wa kuomba kuandaa Michezo ya Afrika ya 2027 na Michezo ya Olimpiki ya 2036 kwa kuzingatia uwezo ambao Misri inamiliki kwa sasa, haswa Mji wa Kimataifa wa Misri kwa Michezo ya Olimpiki, iliyokuwa nguzo ya michezo kwa ulimwengu kwa sababu ya uwezo wake mkubwa na vifaa vilivyotekelezwa na kubuniwa usanifu kulingana na viwango vya juu na vipimo vya kiufundi vya kimataifa, pamoja na msaada endelevu unaoshuhudiwa na mfumo wa michezo wa Misri kutoka kwa Rais Abdel Fattah El-Sisi na ufuatiliaji wake makini wa matukio yote ya michezo yaliyoandaliwa na Misri na mwongozo wa kudumu kwa kutoa mahitaji yote ya mafanikio.

Waziri huyo wa Michezo aliongeza kuwa muundo wa michezo wa Misri kwa sasa unalinganishwa na nchi mbalimbali Duniani, jambo linalotufikisha kuandaa mashindano makubwa ya michezo kama vile Kombe la Dunia la FIFA na Michezo ya Olimpiki.

Kwa upande wake, Dkt. Hassan Mustafa, Mkuu wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Mikono, alisisitiza kuwa Misri ina nafasi kubwa ya kuandaa Michezo ya Olimpiki ya 2036 kutokana na muundo mashuhuri wa ujenzi ambao Misri imeumiliki hivi karibuni, ambao umeifanya kuwa kivutio kwa mashirikisho ya kimataifa kuandaa mashindano makubwa ya kimataifa.

Alibainisha kuwa mnamo kipindi cha miaka mitatu iliyopita, tumeshiriki mashindano 300 ya Barani na Duniani katika michezo yote, yaliyokuwa na athari kubwa katika kufanikisha mashujaa wetu wa michezo nafasi za juu na medali za dhahabu na kuongoza viwango vya dunia katika michezo mingi ya Olimpiki.

Kwa upande wake, Mhandisi Hisham Hatab, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kamati ya Olimpiki ya Misri, alimshukuru Waziri wa Vijana na Michezo kwa uratibu endelevu na Kamati ya Olimpiki katika masuala yote yanayohusiana na mashirikisho ya michezo, na kwa kutoa kila aina ya msaada kwa mashirikisho ili kufikia mafanikio mapya ya Misri katika michezo yote.

Mkutano huo ulipitia hatua za awali za uratibu na Chama cha Kamati za Kitaifa za Olimpiki za Afrika (ANOCA), Umoja wa Siasa za Afrika na Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki kuandaa Michezo ya Afrika ya 2027 na Michezo ya Olimpiki ya 2036, na kukagua utayari wa miundombinu ya michezo ya Misri kuandaa mashindano hayo.

Mkutano huo pia ulipitia majukumu na uwezo wa Kamati ya Kudumu ya Pamoja ya kuandaa utafiti wa kiufundi na kifedha ili kuomba kuandaa hafla kubwa za michezo ya kimataifa, na kuamua mpango kazi mnamo kipindi kijacho kulingana na muda maalum.

Back to top button