Vijana Na Michezo

Udhamini wa Nasser (Kanuni na Masharti)

0:00

Kwa viongozi vijana wanaotarajiwa Duniani kote, salamu kutoka Misri, ardhi ya ustaarabu na historia ya kibinadamu, tunawashukuru kwa nia yenu ya kujiunga kwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa  uliozinduliwa na Wizara ya Vijana na Michezo pamoja na uangalifu wa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri Abdel Fattah El-Sisi.

Katika muktadha huu,tunapenda kusisitiza kwamba uteuzi wa washiriki wa Udhamini wa Nasser unategemea hati na vigezo vingi, navyo ni Maoni ya Misri 2030, Ajenda ya Afrika 2063, Mwenendo wa Umoja wa Afrika wa Uwekezaji kwa Vijana, Mkataba wa Vijana waafrika, Kanuni Kumi za Mkutano wa Bandung, Mkakati wa Ushirikiano wa Kusini-Kusini, Malengo ya Maendeleo Endelevu 2030, Kanuni za Harakati ya kutofungamana kwa Upande Wowote, Hati ya Vijana waafrika katika Amani na Usalama, na Hati ya kiafrika ya Wanawake katika Amani na Usalama, na hati zingine zilizohusiana na kupitishwa ili  kuhakikisha kesho bora kwa wote, kwa kuzingatia tofauti za kijiografia, kielimu, kitaasisi, kiutamaduni, kijamii, kitaaluma,umri na jinsia.

Mapokezi na Malazi

 Wizara ya Vijana na Michezo inashikilia gharama kamili za Malazi, usafiri wa ndani, vyeti, ziara za kiutalii, na vipimo vya Corona( PCR Test) kabla ya saa 48  ya kuondoka Misri, na Washiriki watagharamia tikiti zao za ndege, visa ya kuingia, na vipimo vya Corona(PCR Test) saa 48 kabla ya kusafiri Misri.

Kuhusu Malazi: Washiriki wawili wa mataifa tofauti watawekwa katika chumba kimoja  kwa mujibu wa kanuni za kuishi pamoja na muunganisho iliyopitishwa na Ofisi ya Vijana ya kiafrika ili kuhakikisha kuchanganya na ushirikiano wa kijamii baina ya washiriki katika Udhamini huo.

Maagizo ya Amani  ya COVID-19

Washiriki wote wanaojiandikisha katika Udhamini lazima wapate chanjo dhidi ya COVID-19, Udhamini huo unawataka washiriki wote kuvaa barakoa wakati wote na kudumisha umbali wa angalau mita moja ili kujikinga na wengine, na ikiwa mshiriki ana matatizo ya kiafya yaliyokuwepo awali kama vile magonjwa ya kupumua au magonjwa ya kudumu, lazima abaki chumbani mwake hadi apate nafuu, Vituo vya kusafisha mikono vitatolewa katika maeneo yote, ikiwa ni pamoja na vyumba na kumbi za  mikutano.

Faragha na sera

Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa “Udhamini” una jukumu katika kulinda faragha na data ya waombaji. yafuatayo yanafafanua sera ya faragha, na jinsi tunavyokusanya, kutumia, kuhifadhi na kulinda taarifa zako za kibinafsi.

Kukusanya Data

Udhamini hukusanya taarifa za kibinafsi kutoka kwa waombaji wanapojaza fomu ya kujiunga na Udhamini, ikiwa ni pamoja na jina, maelezo ya mawasiliano, elimu, uzoefu wa kazi na taarifa nyingine muhimu.na pia tunaweza kukusanya maelezo zaidi kutoka kwa waombaji wakati wa kuwasilisha maombi au wakati wa ushiriki wao katika Udhamini ikiwa ni lazima.

Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa  unamiliki maudhui yote yaliyochapishwa katika tovuti yake, ikiwa ni pamoja na maandishi, picha, video na vyombo vingine vya habari. Maudhui hayo yote yanalindwa na haki za kunakili na hayawezi kutolewa tena au kusambazwa bila idhini ya maandishi kutoka Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa.

Matumizi ya Data

Udhamini hutumia data zilizokusanywa ili kutathmini maombi na kuchagua wenzao kwa  programu yetu. Pia tunaweza kutumia data zilizokusanywa kuwasiliana na waombaji kuhusu fursa za siku zijazo au programu zingine zinazofaa.pia inafaa kutaja kwamba Udhamini hauuzi au kushiriki data ya mwombaji na wakala wowote wa kibiashara au uuzaji timu ya udhamini ina  haki ya kutumia na kuchapisha video yoyote iliyowasilishwa kwetu kwenye majukwaa yetu na chaneli za mitandao ya kijamii,kwa sharti kwamba tunazingatia  maudhui yaliyomo  yanafaa,na hii haimaanishi kukubalika katika programu ya Udhamini.

Kuhifadhi data

Tunachukua hatua zinazofaa ili kulinda dhidi ya ufikiaji usioidhinishwa, ubadilishaji, ufichuzi usioidhinishwa au uharibifu wa data, Hatua hizi ni pamoja na ukaguzi wa ndani wa ukusanyaji wa data, uhifadhi na kuchakata na hatua za usalama.

Mabadiliko katika Sera ya Faragha

Udhamini unahifadhi haki ya kusasisha Sera ya Faragha wakati wowote  bila kutoa taarifa, na mabadiliko yoyote au masasisho yatachapishwa kwenye jukwaa letu ili kila wakati uwe na ufahamu wa taarifa tunazokusanya na jinsi tunavyozitumia.

Tume ya uteuzi inahifadhi haki ya kukataa maombi yoyote bila maelezo.

Mmoja kwa ajili ya Wote, Wote kwa ajili ya Mmoja.

Back to top button