Habari Tofauti

Imamu Mkuu afungua Taasisi ya Azhar kwa kufundisha Kiarabu kwa wazungumzaji wasio asilia huko mji wa Nasr

Mervet Sakr

0:00

Mtukufu Imamu Prof. Ahmed Al-Tayeb, Sheikh wa Al-Azhar Al-Shareif, alizindua Taasisi ya Al-Azhar ya Kufundisha Lugha ya Kiarabu kwa Wazungumzaji Wasio asilia katika Wilaya ya sita ya Mji wa Nasr,kwa mahudhurio ya Dkt. Muhammad Al-Dwaini, Naibu Al-Azhar Al-Shareif, na Dkt. Nahla Al-Saidi, Mshauri wa Sheikh wa Al-Azhar kwa masuala ya Ughaibuni,na Sheikh Ayman Abdul Ghani, mkuu wa sekta ya taasisi za Al-Azhar, na kundi la viongozi wakuu katika Al-Azhar Al-Shareif.

Dkt. Nahla Al-Saidi aliwasilisha kwa Mtukufu baadhi ya maelezo kuhusiana na madhumuni ya kuanzishwa kwa taasisi hiyo, nguzo zake na mkakati wa ufundishaji hapo, akifafanua kuwa taasisi hiyo iko kwenye eneo la takriban mita za mraba 1,000, na inajumuisha sakafu 4; Ina vyumba vya madarasa 17 vyenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 360 na kundi la ofisi za utawala, vyumba vya mikutano, msikiti, maktaba, maabara ya kompyuta, ukumbi wa michezo na ukumbi wa semina.

Mtukufu Imamu Mkuu, alitoa Shukrani zake kwa nafasi ya Kituo cha Maendeleo ya Elimu kwa Wanafunzi wa Kimataifa na Kigeni huko Al-Azhar, na juhudi zake katika kufuatilia uanzishaji, usanifu na utoaji wa taasisi hiyo, pamoja na mbinu za kisasa za teknolojia zinazotumika katika nyanja za elimu, msaada kwa wanafunzi wa kigeni na wa kimataifa, kukidhi mahitaji yao na kuboresha uwezo wao wa kielimu na kiutamaduni ndani ya mpango mkakati wa Kituo, unaolenga kupanua taasisi za kufundisha lugha ya Kiarabu kwa wazungumzaji wasio asilia.

Taasisi hiyo inafanya kazi pamoja na usimamizi wa Kituo cha Maendeleo ya Elimu kwa Wanafunzi wa Kigeni na huko Al-Azhar Al-Sharif.

Back to top button
اكتب رسالتك هنا
1
تواصل معنا
اهلا بك في بوابة " مصر الآن"