Vijana Na Michezo

Uwanja  wa  Alexandria

0:00

Ni uwanja mwenye matumizi mbali mbali, amabao uko mjini Alexandria katika Mtaa wa Muharam Bik nchini Misri, lakini hivi sasa unatumiwa katika mechi za mpira wa miguu.

Uwanja  huu  ni  uwanja  rasmi  wa  Timu  ya  Al-Itihad, Timu  ya  Al-Olimb i na  Timu  ya  Sumuha.

Uwanja  wa  Alexandria  ni  uwanja  wa  zamani  sana  nchini  Misri  na  katika  Afrika, licha  ya  kuwa  ni  uwanja  wa  kwanza  katika  Ulemwengu  wa  Kiarabu  kutumia  taa.

Uwanja  huo  ulijengwa  mwaka  1929,  ambapo  ulikuw  na  upana  wa  kukaliwa  na mashabiki  13660,  lakini  baada  ya  marekebisho  ukawa  na  uwezo  wa  kukaliwa na  mashabiki  20000.  Uwanja huo umefunguliwa  mnamo  17  Novemba  1929, wakati  huu  uliitwa  Uwanja  wa  Fuaad  Al-Awal.  Mfalme  Fuaad  Al-awal amehudhuria  ufunguzi  wake  kupitia   mechi   iliyofanyika  kati  ya  Timu  ya    Al-Itihad na Timu ya Cairo.

Baada ya Mapinduzi ya Julai 1952, limebadilika jina la uwanja na likawa Uwanja wa Al-Baladia,  kisha  limebadilika  na  likawa  Uwanja wa Alexandria (jina la hivi  sasa ).

Ulipoanzishwa ramani yake ilikuwa kwa Msanifu ujenzi wa kirusi Nikosov  ambaye amechora  ramani  ya  uwanja,  ramani  yenye  kufanana  na  nembo  za  ushindi  za  kigiriki  kwa  mfumo  zamani   wa  kirumi, lakini  kwa  njia  ya  kisasa.

Vile vile alichunga kuwa ramani ya uwanja kukusanya baadhi ya sehemu za kuta za mji wa zamani wa kiislamu Alexandria.

Uwanja huo umesharekebishwa mwaka 1996  kabla  ya  Michuano  ya  Kombe  la  Dunia  kwa  Vijana, ambapo  zimefanyika  huko  baadhi  ya  mechi  za  michuano  hiyo.

Pia umerekebishwa kabla ya Michuano ya Kombe la Mataifa ya Kiafrika mwaka  2006, ambayo timu ya Misri  ilikuwa  bingwa  wa  kombe  hilo.

Vile vile  umesharekebishwa  kabla  ya  ufunguzi   wa   Michuano  ya  Klabu  Bingwa  za  Kiarabu,  michuano  iliyofanyika  nchini  Misri  kwenye  miji  miwili  nayo  ni ; Alexandria  na  kairo.

Back to top button
اكتب رسالتك هنا
1
تواصل معنا
اهلا بك في بوابة " مصر الآن"