Habari

RAIS DK.MWINYI AKUTANA NA MTENDAJI MKUU WA MAKUMBUSHO YA OMAN

0:00

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amekutana na Mtendaji Mkuu wa Makumbusho ya Taifa ya Oman Jamal al-Moosawi na ujumbe wake Ikulu Zanzibar leo tarehe 10 Oktoba 2023.

Rais Dk.Mwinyi amemkaribisha Jamal al-Moosawi Zanzibar kwa fursa za kuendeleza ushirikiano katika nyanja tofauti za kihistoria, uhifadhi wa mali kale na Serikali iko tayari kutoa ushirikiano.

Pia mazungumzo yao wamegusia fursa mbalimbali za uhifadhi wa mali kale kwa kubadilishana uzoefu ,elimu pamoja na mafunzo ya kujenga uwezo.

Jamal al-Moosawi  yuko nchini kujionea historia na uhifadhi wa mali kale na makumbusho Tanzania ikiwa ni sehemu ya kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na Oman.

Back to top button