Habari

RAIS DK.MWINYI ASEMA SMZ ITAENDELEZA USHIRIKIANO NA KUJIFUNZA KUTOKA SMT

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendeleza ushirikiano uliopo na kujifunza zaidi kati ya Wizara pamoja na Taasisi zake za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ameyasema hayo  alipokutana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais , Mipango na Uwekezaji  Mhe.Prof Kitila Mkumbo aliyefika Ikulu Zanzibar na ujumbe wake leo tarehe 05 Agosti, 2023.

Aidha, Rais Dk.Mwinyi amewapongeza na kuwashukuru  ujumbe huo kwa  utayari wa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mawazo ya kimageuzi yanalolenga kujenga uchumi wa wananchi wa pande zote mbili katika ushirikiano wa Taasisi zinazohusu Mamlaka ya Bandari, Ofisi ya Msajili Hazina, Mamlaka za Uwekezaji pamoja na Tume ya Mipango ya Taifa .

Ujumbe ulioongozana na Waziri Prof.Kitila pamoja na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji  Dk.Tausi Kida, Msajili wa Hazina Nehemia Mchechu, Katibu wa Tume ya Mipango Lawrence Mafuru, Mkurugenzi Mkuu EPZA Charles Itembe, Mkurugenzi Mkuu TIC Gilead Teri na Mkurugenzi wa Miundombinu TPA Dk.Hussein Lufunyo.

Back to top button