Habari

DKT.MWINYI AWAOMBA SEKTA BINAFSI KUWALIPA MISHAHARA WATUMISHI KABLA YA IDD, ATOA MILIONI 5 KWA WASHINDI WA QURAN NA KUKABIDHI GARI

Mervet Sakr

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi amewaomba Sekta binafsi Zanzibar kuwalipa mishahara watumishi wao wa sekta hizo leo na kesho  kabla ya Sikukuu ya Idd.

Ameyasema hayo leo tarehe 19 Aprili 2023 katika fainali za mashindano ya Quran kwa njia ya Tar-til yalioandaliwa na Shirika la utangazaji Zanzibar (ZBC) kwa kushirikiana na ofisi ya  Mufti mkuu Zanzibar yaliyofanyika ukumbi wa Golden Tulip Airport, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Aidha Rais Alhaji Dk.Mwinyi amewakumbusha Wazazi na Walezi katika kipindi hiki cha sasa kukabiliana na vitendo vya mmong’onyoko wa maadili kwa kuwaweka karibu  Watoto na kusimamia nyendo zao katika kuwaandaa Vijana kuwa raia wema na wenye hofu kwa Mwenyezi Mungu.

Rais Dk.Mwinyi amekabidhi zawadi kwa mshindi wa kwanza Said Juma kutoka Mkoa wa Mjini Magharibi  gari Toyota Alphard .

Mshindi wa pili Nassor Kombo zawadi  ya pikipiki na mshindi wa tatu Zakariya Sheha  shilingi milioni mbili .

Pia Rais Dk.Mwinyi ametoa  shilingi milioni tano kwa mshindi wa nne mpaka wa nane wa fainali hizo.

Back to top button