Habari Tofauti

Rais Hussein Ali: Serikali itaweka Kipaumbele katika Bajeti ya Sekta ya Elimu kutokana na Mchango mkubwa wa Sekta hiyo kwa Taifa

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itaweka Kipaumbele katika Bajeti ya Sekta ya Elimu kutokana na Mchango mkubwa wa Sekta hiyo kwa Taifa.

Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Chama cha Walimu Zanzibar ZATU ulioambatana na Uchaguzi wa Viongozi wa Chama nicho ambao ulifanyika Katika Ukumbi Wa ZSSF Tibirinzi Chake Chake Pemba.

Amesema Bajeti ya Serikali pamoja na vyanzo vyengine vya fedha vitakavyosaidia kuimarisha Sekta ya Elimu vitaelekezwa katika ununuzi wa Thamani, Vitabu, Ajira kwa waalimu, pamoja na vitu vyote ambavyo vitasaidia kufundishia.

Akifafanua umuhimu wa Serikali kuweka kipaombele katika Sekta ya Elimu Mh. Rais amesema nidhahiri kuwa haja ya kufanya hivyo ni kubwa kwa sekta hiyo kutokana na ongezeko la Watoto wanaohitaji kupata Elimu Ambayo ni Haki yao.

Wakati huo huo Dk Mwinyi amewataka Waalimu Kuimarisha Uhusiano Kati yao na Wazazi wa Wanafunzi kwa kuwahimiza kuimarisha Malezi ya Pamoja , kwa watoto ili kuwajengea Maendeleo na Mustakbali Mwema Wa Maisha ya Sasa na ya Baadae.

Aidha amewataka Waalimu kuona Umuhimu wa kuzitumia Fursa mbali mbali zilizopo za Kujiendeleza kielimu ili kuweza kupata Maarifa Mapya ya kufundishia Wanafunzi kwa Uweledi Zaidi na kuweza kujijengea Heshima Kwa Jamii.

Akizungumzia Suala la Uchaguzi wa Viongozi wa Chama Cha Waalimu Zanzibar ZATU Dk Hussein amewataka Wanachama wa Chama hicho amabao ni Walimu kuwa Makini katika Kuchagua Viongozi bora watakaofanikisha kusogeza mbele Maendeleo ya Chama cha Waalimu.

Akijibu baadhinya Mapendekezo yaliyotolewa na Chama hicho amesema kuwa Serikali italifanyia kazi ombi lilitolewa na Waalimu juu ya kupata Tume Maalum ya Utumishi Serikalini kwa Waalimu ambayo itasaidia kuimarisha Maslahi ya Waalimu Nchini.

Awali Akitoa salam za Wizara katika Kilele cha Siku hiyo ya Waalimu Duniani Waziri Wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh.Leila Muhammed Mussa amewataka Waalimu Wakuu nchini kusimamia Mitaala Mipya iliyofanyiwa marekebisho kwa Wanafunzi wa Skuli za Maandalizi na Msingi.

Aidha Waziri Leila amewaomba waalimu kuendelea kujiunga na Chama hicho ili kukizidishia uhai ambao utasaidia katika kutatua changamoto mbali mbali zinazowakabili waalimu kwa urahisi.

Akisoma Risala kwa niaba ya Chama cha Waalimu Zanzibar ZATU Katibu Mkuu wa Chama hicho Haji Juma Omar amesema kuwa Chama kimeweka Mikakati Endelevu ya Miaka 5 ikiwemo kujadili Maendeleo ya Chama hicho, Kuchagua Viongozi wapya, ambao watahimiza uwajibikaji kwa Waalimu, pamoja na kuunga Mkono juhudi zinazoendelea kufanywa na Serikali ya Awamu ya Nane katika Kukuza maendeleo ya Elimu.

Huu ni Mkutano Mkuu wa 8 wa Chama cha Walimu Zanzibar ZATU ambao kwa mwaka huu umeambatana na Uchaguzi wa Viongozi wa Chama hicho.

 

زر الذهاب إلى الأعلى