Uchumi

Wajasiriamali nchini wahimizwa kuweka akiba Benki ya Mwanga Hakika

WAJASIRIAMALI na wafanyabiashara nchini wameombwa kujitokeza kwa wingi kuweka akiba katika benki ya Mwanga Hakika waweze kupata asilimia 12 ya faida kwa kipindi cha miezi sita hadi mwaka mmoja Maisha ni Mseleleko.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wakubwa katika benki ya Mwanga Hakika, Projest Massawe, amesema kuwa benki hiyo ina kampeni ya benki iitwayo ‘Jipange sasa Maisha ni Mseleleko’.

Massawe amesema ili kuhakikisha wanawafikia wateja wengi zaidi benki imeamua kima cha chini cha uwekezaji ni kuanzia Sh 500,000 na kuendelea na kwamba kila kiwango atakachoweka mteja kitampati fursa ya kupata faida mpaka asilimia 12 kwa kipindi cha miezi sita hadi mwaka mmoja.

“Mteja atakayeweka amana katika benki yetu kwa kipindi cha miezi sita hadi 12 atapata faida mpaka asilimia 12 kwa mwaka, tumekuja na kampeni hii ya Mseleleko Akaunti ambayo itakuwa ya miezi mitatu tunategemea tutawagusa watanzania wengi.

“Kwenye hii fursa ya kuweka akiba katika benki yetu na kupata gawio au faida mpaka asilimia 12 kwa kipindi cha mwaka mmoja,” amesema Massawe.

Amesema benki hiyo kwa sasa ina matawi saba nchi nzima, itaweza kuwahudumia watanzania wote hata wale ambao bado matawi hayajafika kwa kutumia mtandao na simu banki.

“Mkakati wetu ni kuwekeza kwa wafanyabiashara na ndio maana tupo hapa kulihamasisha kundi hilo kuja na kupata faida ikiwemo ya kupata mkopo hadi asilimia 80 ya fedha ambayo amewekeza hapa kwetu,” amesema Massawe.

Pia ameongeza kwa kuishukuru serikali kwa kuweka mazingira wezeshi kwa taasisi za kifedha ikiwemo benki yao kuweza kuwahudumia wateja mbalimbali na kuwasaidia kuweza kukuza uchumi wao kupitia uwekezaji.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Biashara Wateja wa kati na wadogo katika benki hiyo, Joseph Samson amesema kwa mfanyabiashara au mjasiriamali atakayeweka akiba katika benki yao, moja ya kigezo anachotakiwa kuwa nacho ni awe mtu anayefanya shughuli inayokubalika na serikali.

 

زر الذهاب إلى الأعلى