Habari Tofauti

TOENI MOTISHA KWA WATOA HUDUMA ZA AFYA

 

Viongozi katika  vituo vya kutolea huduma za afya  nchini wameelekezwa  kutoa motisha kwa wafanyakazi wanaofanya  vizuri ili kuwapa  ari  ya  kufanya kazi kwa bidii  ya kutoa huduma bora kwa jamii.

Maelekezo hayo yametolewa na Dkt.Ntuli Kapologwe Mkurugenzi wa Idara ya  afya, Ustawi  wa Jamii na Lishe kutoka Ofisi ya Rais Tawala Za Mikoa na Serikali za Mitaa ( TAMISEMI) wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara ya tathmini na ukaguzi katika  Mkoa wa Mwanza kilichofanyika katika ofisi za mkuu wa mkoa wa Mwanza.

“Viongozi wenzangu Waganga wakuu wa Mikoa na Wilaya hakikisheni mnaweka utaratibu wa kutoa motisha kwa watoa huduma za afya katika maeneo yenu lengo likiwa ni kuzidi kuwatia ari na Motisha ya kuwahudumia Wananchi.” amesisitiza Dkt.Ntuli.

Amefafanua  kuwa  Zawadi sio fedha ,pekee bali wanaweza kuweka utaratibu  wa kutoa  vyeti au  kuwaandikia barua za pongezi na kutambua michango yao kwenye sekta kwa kuwa  itawapa nguvu zaidi ya kufanya kazi kwa bidii.

Aidha, amewataka viongozi hao  kutekeleza maelekezo hayo na kutoa  mrejesho.

زر الذهاب إلى الأعلى