Habari

Dkt. Hussein Mwinyi: Malengo ya Mkutano wa Wadau wa Biashara ya Utalii (Z- Summit) unalenga kutangaza fursa

Ahmed Hassan

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema malengo ya Mkutano wa Wadau wa Biashara ya Utalii (Z- Summit) unalenga kutangaza fursa na kukuza zaidi utalii za Zanzibar.

Dkt.Mwinyi amesema Serikali inajitahidi kuweka mazingira ya kuvutia zaidi ya Uwekezaji Zanzibar ili kuifanya Zanzibar kuwa kivutio cha wawekezaji na watalii na kuepuka athari za mazingira kwenye rasilimali zetu za Visiwa.

Sekta ya utalii duniani inachangia uchafuzi wa mazingira, upotevu wa viumbe hai, mabadiliko ya tabia ya nchi, hewa na maji hivyo tushikamane kuhakikisha Zanzibar ibaki na uhifadhi mzuri wa mazingira.

Dkt.Mwinyi amesema Utalii unachangia kwa kiasi kikubwa uchumi wa Zanzibar kwa karibu asilimia 30 %. Hivyo Serikali imejitolea kukidhi mahitaji ya soko la utalii kwa kujipanga kwa kufikia idadi ya watalii 850,000 ifikapo 2025.

Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo alipozindua Mkutano wa Wadau wa Biashara ya Utalii (Z- Summit) uliofanyika Hoteli ya Golden Tulip Aiport Zanzibar.

Kabla ya kuzindua mkutano huo Rais Dkt. Mwinyi alitembelea mabanda ya wadau mbalimbali wa Utalii kutoka ndani na nje ya nchi.

زر الذهاب إلى الأعلى