Habari

SERIKALI IMEINGIZA BILIONI 32 KWA MAKUSANYO MWAKA UWANJA WA NDEGE ZANZIBAR

Ahmed Hassan

Rais wa Zanzibar Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi kampuni zilizokuwa zikiendesha huduma za uwanja wa ndege wa Abeid Amani Karume kwa zaidi ya miaka 25, uwanja huo ulikuwa ukipata hasara pamoja na Serikali kulipa mishahara ya wafanyakazi wa uwanja huo. Baada ya kampuni ya Dnata kuanza kazi kwa mwezi wa disemba (robo ya mwisho wa mwaka) uwanja huo umekusanya Shilingi bilioni 8.1 ambapo wastani kwa mwaka ni shilingi bilioni 32.

Kwa upande wa makusanyo ya fedha za maegesho ya magari uwanja wa ndege ulikuwa ukipata shilingi milioni 2 ikilinganishwa na hivi sasa kwa mwezi wa januari Serikali imekusanya shilingi milioni 139.

Rais Dk.Mwinyi aliyasema hayo alipokutana na waandishi wa habari Ikulu Zanzibar leo tarehe 28 Februari 2023.

Back to top button