Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi ametembelea eneo la Shehia ya Kama Wilaya ya Magharibi A, Mkoa wa Mjini Magharibi kukagua ujenzi wa mradi wa mfereji mkubwa wa maji ambao ulikuwa kero ya muda mrefu.
Wananchi wa Shehia hiyo walimshukuru Rais Dkt. Mwinyi kwa kutekeleza ahadi na kutatua changamoto hiyo sugu ambayo imedumu kwa muda mrefu, mradi huo unatarajiwa kumalizika kabla ya msimu wa mvua.
Wakati huo huo Rais Dkt. Mwinyi alitembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Masoko ya kisasa maeneo ya Chuini kwa Nyanya, Soko la Jumbi na Mwanakwerekwe.
Dkt.Mwinyi amewaagiza wakandarasi wa Masoko hayo kukamilisha ujenzi ifikapo Mwezi Novemba ili kuyafungua Disemba Mwaka huu.