Habari Tofauti
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanziba amesema idadi ya ufaulu kwa Wanafunzi wa kidato Cha nne kwa Skuli za Zanzibar umeengezeka kwa asilimia 6.1
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Lela Muhamed Mussa amesema idadi ya ufaulu kwa Wanafunzi wa kidato Cha nne kwa Skuli za Zanzibar umeengezeka kwa asilimia 6.1 ikilinganishwa na matokeo ya mwaka 2021.
Amesema hayo wakati akitoa taarifa ya tathmini ya matokeo ya kidato Cha nne kwa Skuli za serikali na Skuli binafsi kwa wandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo Mazizini Unguja amesema ufaulu umeengezeka hasa Kwa Wanafunzi wa kike.
Amesema kutokana na idadi kubwa ya ufaulu Serikali itaongeza madarasa ya kidato cash Tano kwa Skuli ya Sekondari Mahonda Mkoa wa Kaskazini Unguja na Skuli ya Hasnuu Makame kwa Mkoa wa Kusini Unguja.
Amesema lengo la kuongeza madarasa hayo ni kurahisisha mazingira ya kusoma kwa Wanafunzi.
Aidha Mhe Lela kwa mujibu wa matokeo hayo baraza la Mitihani Tanzania imeifungia Skuli ya mnemonic academy ya Mjini Magharib kwa kuthibitika kupanga na kufanya udanganyifu Katika mitihani.