Waziri wa Mambo ya Nje ampokea Waziri wa Mambo ya Nje wa Somalia
Jumamosi, Juni 29, Balozi Ahmed Abu Zeid, Msemaji rasmi wa Wizara ya Mambo ya Nje, alisema kuwa Waziri wa Mambo ya Nje Sameh Shoukry alimpokea Bw.Ahmed Moalim Faki, Waziri wa Mambo ya Nje wa Somalia, ambapo mkutano ulishughulikia masuala mbalimbali ya mahusiano ya Misri na Somalia na njia za kuimarisha na kuendeleza katika nyanja mbalimbali.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje alieleza kuwa mazungumzo hayo yalishughulikia mipango ya ushirikiano iliyopo kati ya nchi hizo mbili katika nyanja za mafunzo, usafiri wa anga, afya, elimu na utamaduni, ambapo mawaziri hao wawili walionesha furaha yao kwa tangazo la ufunguzi wa safari ya moja kwa moja ya ndege kati ya nchi hizo mbili Julai ijayo, pamoja na ufunguzi wa tawi la Banque Misr nchini Somalia.
Kwa upande mwingine, Balozi Abu Zeid alifichua kuwa mkutano huo uligusia hali ya kikanda katika Pembe ya Afrika, ambapo mawaziri wa mambo ya nje wa nchi hizo mbili walibadilishana mashauriano na uratibu kuhusu maendeleo muhimu zaidi katika suala hili, na kusisitiza nia yao ya kusaidia utulivu na amani na kuepuka vyanzo vya mvutano na uharibifu.
Mwishoni mwa mkutano huo, walisisitiza umuhimu wa mahusiano kati ya Misri na Somalia na nia ya pande zote mbili ili kuziendeleza na kuziimarisha katika hatua inayofuata.