Habari

DKT.MWINYI APOKEA TUZO YA VIP GLOBAL WATER CHANGEMAKERS AWARD 2023

Ahmed Hassan

0:00

 

RAIS DK.MWINYI APOKEA TUZO YA VIP GLOBAL WATER CHANGEMAKERS AWARD 2023, KUIFANYA ZANZIBAR KUWA NCHI YA KWANZA KUANDAA PROGRAMU YA UWEKEZAJI WA MAJI AFRIKA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema: Ni heshima kubwa kutunukiwa tuzo kwa niaba ya Serikali na Wananchi ikiwa ni jitihada za Serikali kuimarisha huduma za maji Zanzibar kwa mabadiliko na mageuzi kwenye sekta hiyo.

Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo leo Ikulu Zanzibar baada ya kupokea Tuzo maalumu iitwayo kama VIP Global Water Changemakers Awards 2023 kutoka kwa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Bodi ya Ushirika wa Maji Duniani Kusini mwa Afrika, Mwenyekiti wa Kitengo cha Uratibu Afrika Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.

Tuzo hiyo imetolewa wakati wa mkutano wa maji wa Umoja wa Mataifa tarehe: 22 Machi 2023 jijini New York, Marekani.

Dk.Mwinyi amesema tuzo hiyo imetokana na Zanzibar kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kuandaa na kuzindua Programu ya uwekezaji katika sekta ya maji ambayo inajulikana kama Zanzibar Water Investment Programme ya mwaka 2022-2027 iliyozinduliwa mpango rasmi tarehe 11 Machi 2022 katika Kongamano la uwekezaji wa sekta ya maji barani Afrika lililofanyika Hoteli ya Melia Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Naye, Rais Mstaafu Dkt. Kikwete amesema tuzo hiyo imeipa heshima Zanzibar Kimataifa na pia ni ishara kuwa Jumuiya za Kimataifa zimetambua jitihada zinazofanywa na Rais Dk. Mwinyi katika kuendeleza sekta ya maji Unguja na Pemba.

Back to top button