UMISSETA YAINGIA SIKU YA NNE TABORA
Mashindano ya Umoja wa Michezo ya Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA 2023) yameingia siku ya nne Mkoani Tabora yanakofanyika kitaifa, huku timu kutoka mikoa mbalimbali zikiendelea kushindana katika michezo tofauti.
Michezo iliyochezwa leo Tarehe 18 Juni 2023 ni pamoja na Riadha Wasichana na Wavulana iliyoanza mapema Saa 12 Alfajiri, Soka Wasichana na Wavulana, Netiboli, Kikapu Wasichana na wavulana, Mpira wa mikono, Wavu, Sanaa za Michezo pamoja na Mpira wa Meza.
Upande wa Riadha imefikia hatua ya nusu fainali kwenye mita 100, 200 na 1,500, huku fainali zikitarajiwa kuanza tarehe 20 Juni 2023 katika mchezo huo ambao umeonesha kuwa na upinzani mkali kutokana na mikoa mbalimbali kuonekana kujiandaa vizuri.
Siku ya nne ya UMISSETA pia imeshuhudia Mchezo wa Mpira wa Meza (Table Tennis) mikoa ya Tabora, Mwanza, Dar es salaam, Unguja, Singida, Njombe, Morogoro na Simiyu ikiibuka na Ushindi katika michezo yao.
Soka wasichana Shinyanga imeifunga Katavi 4-0, Mwanza ikaifunga Tanga 3-0, Geita na Dar es salaam zikatoshana nguvu baada ya kwenda sare ya 2-2 naa badae Mara ikaifunga Lindi 3-0.
Katika mchezo mwingine wa Soka Wasichana uliochezwa kwenye uwanja A wa Sekondari Tabora Wavulana, Kagera iliifunga Songwe 3-2, Kilimanjaro na Pwani zikashindwa kutambiana baada ya kutoka sare ya 1-1 na baadae Mbeya ikakutana na Mtwara matokeo yakiwa 1-0.
Katika mpira wa Wavu Timu ya Kanda ya Unguja Wavulana iliifunga Ruvuma kwa Seti 3-0, Rukwa ikaifunga Iringa 3-1, Kigoma ikaifunga Simiyu 3-0, Katavi ikakubali kufungwa na wenyeji Tabora kwa 3-0 na Tanga ikaifunga Singida 3-0.
Wavu Wasichana matokeo yaliisha kwa Singida kuifunga Simiyu Seti 3-0, Shinyanga ikaifunga Njombe 3-0, Tabora ikakubali kipigo cha 3-2 kutoka kwa Manyara na Dar es salaam ikaifunga Kigoma 3-0.
Michezo ya Netiboli iliyochezwa Viwanja A na B shule ya Sekondari Tabora wasichana Asubuhi Tare 18 Juni 2023 Kilimanjaro iliifunga Rukwa 33-16, Mbeya ikaifunga Ruvuma 43-21, Njombe.