Habari

Waziri wa Mambo ya Nje ampokea Waziri wa Nchi wa Uingereza kwa Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini

Mervet Sakr

Waziri wa Mambo ya Nje Sameh Shoukry Aprili 4, alipokea Lord Tariq Ahmed, Waziri wa Nchi wa Uingereza wa Mashariki ya Kati, Afrika Kaskazini, Asia Kusini na Umoja wa Mataifa katika Ofisi ya Mambo ya Nje, Jumuiya ya Madola na Maendeleo ya Uingereza.

Balozi Ahmed Abu Zeid, Msemaji Rasmi na Mkurugenzi wa Idara ya Diplomasia ya Umma katika Wizara ya Mambo ya Nje, alisema kuwa ziara hii ya pande mbili inakuja ndani ya muktadha wa umakini wa pamoja ili kuimarisha mifumo ya ushirikiano wa pamoja na uratibu kati ya Misri na Uingereza katika nyanja mbalimbali, na kujenga matokeo ya mkutano wa kwanza wa Baraza la Ushirikano kati ya nchi hizo mbili, uliofanyika Julai mwaka jana jijini London, ambapo Waziri Shoukry alianza mkutano huo kwa kumkaribisha mgeni rasmi, akipongeza nia ya upande wa Uingereza katika kuimarisha mifumo ya mazungumzo na Misri kuhusu mada mbalimbali zenye maslahi ya pamoja, hivyo kuchangia kuimarisha maeneo ya kazi ya pamoja.

Msemaji huyo aliongeza kuwa mazungumzo hayo yanaonesha wazi mahusiano maarufu ya kihistoria kati ya nchi hizo mbili, kwani mawaziri hao wawili walisisitizia umuhimu wa kuendeleza mifumo ya mashauriano ya kiufundi ili kujiandaa kwa kikao cha pili cha Baraza la Ushiriki mjini Kairo mwaka huu pamoja nan uenyekiti wa mawaziri hao wawili wa mambo ya nje, na pia kushughulikia masuala mbalimbali ya ushirikiano baina ya nchi hizo mbili, haswa uchumi na biashara. Katika muktadha huo, Waziri Shoukry alitathmini kiasi cha uwekezaji wa Uingereza katika soko la Misri na nafasi ya kwanza ya Uingereza katika orodha ya uwekezaji wa kigeni nchini Misri, akisisitiza nia ya serikali ya Misri katika kuongeza uwekezaji huo na kuimarisha ushiriki wa kampuni za Uingereza katika miradi mikubwa ya kitaifa nchini Misri, pamoja na kuongeza kiwango cha ubadilishanaji wa biashara kati ya nchi hizo mbili ili kufikia maslahi yao, pamoja na kutafuta fursa zaidi za ushirikiano wa nchi mbili.

Katika suala hili, Waziri Shoukry na Waziri wa Nchi wa Uingereza walijadili athari za mgogoro wa sasa wa kiuchumi Duniani, na njia za ushirikiano ili kupunguza athari za mgogoro huo, ambapo Shoukry alisisitiza umuhimu wa juhudi za pamoja za kimataifa za kutoa msaada kwa nchi zinazoendelea zilizoathiriwa zaidi na mgogoro huo ili kudhibiti athari zake mbaya, haswa kwenye minyororo ya usambazaji wa chakula.

Balozi Abu Zeid ameongeza kuwa mawaziri hao wawili walibadilishana maoni juu ya masuala kadhaa ya kikanda na kimataifa, ikiwa ni pamoja na athari za mzozo wa Urusi na Ukraine, kuongezeka kwa maeneo ya Wapalestina, pamoja na maendeleo ya hivi karibuni katika eneo la Libya, faili la Syria, na hali ya Sudan na Yemen. Waziri Shoukry alikuwa na nia ya kumjulisha Waziri wa Nchi wa Uingereza juu ya uamuzi wa misimamo ya Misri juu ya faili hizi na juhudi za Misri za kufikia utulivu unaotakiwa katika eneo hilo. Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza alielezea nia ya nchi yake katika kuendeleza mahusiano na Misri, kwa kuzingatia umuhimu wake kama mshirika wa kimkakati wa Uingereza, akisifu katika suala hili jukumu la Misri katika kusaidia nguzo za usalama na utulivu katika Mashariki ya Kati.

Mwishoni mwa mkutano huo, Waziri Shoukry na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza walikubaliana juu ya umuhimu wa kuendelea kufanya kazi pamoja kusonga mbele mahusiano kati ya Misri na Uingereza, na kuimarisha utaratibu wa mashauriano na uratibu juu ya masuala ya kipaumbele katika eneo hilo.

زر الذهاب إلى الأعلى