Habari Tofauti

Tanzania na UNESCO kushirikiana zaidi katika masuala ya maji

Ahmed Hassan

0:00

Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso (Mb) amefanya kikao na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bw. Xing Qu katika ofisi za UNESCO jijini New York, Marekani kwa lengo la kujadiliana kuhusu ushirikiano katika usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za maji, na maji shirikishi.
Waziri Aweso amewasilisha ombi la Tanzania ikiwano kujengewa uwezo na UNESCO katika usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za maji na utekelezaji wa miradi ya maji, na kuandaa maandiko mbalimbali kuhusu rasilimali za maji na miradi.
Naye Naibu Mkurugenzi mkuu UNESCO Bw. Xing Qu ameahidi ushirikiano katika maeneo ya kipaumbele kwa Afrika ikiwemo usimamizi wa masuala ya maji, na kujenga uwezo wa taasisi katika tathmini ya usimamizi wa Rasilimali za Maji.
Back to top button