Vijana Na Michezo

Wizara ya Vijana na Michezo yaandaa mradi wa kitaifa “Maadili Yangu Yaniashiria” katika Kituo cha Olimpiki cha mafunzo ya timu za kitaifa huko Maadi

Ali Mahmoud

Wizara ya Vijana na Michezo-Idara Kuu ya maendeleo ya vijana wachanga, Idara Kuu ya malezi ya shule, kwa uratibu na Idara Kuu ya shughuli za wanafunzi katika Wizara ya Elimu, na Shirikisho la Michezo kwa wote, yanaandaa mradi wa kitaifa wa kueneza moyo wa uaminifu na ushiriki na kuendeleza mwelekeo wa kidini na maadili ikiwa na kichwa cha “Maadili yangu Yaniashiria” mnamo kipindi cha kuanzia Februari 25 hadi machi 17, 2023 katika Kituo cha Olimpiki cha Mafunzo ya Timu za Kitaifa huko Maadi.

Ambapo shughuli za awamu ya kwanza hufanyika kwa ushiriki wa vijana kutoka kwa mikoa ya (Kairo – Giza – Qalyubia) na wanafunzi 750 wa kiume na wa kike kutoka kidato cha shule ya kimsingi na za elimu ya kiakili, wanashiriki katika mpango huo, lakini awamu moja inapaswa kuwa kwa ushiriki wa wanafunzi 250 wa kiume na wa kike.

Mpango huo unalenga kuelimisha vijana wachipukizi kuhusu jinsi ya kunufaika na jukumu chanya la mitandao ya kijamii, kukuza mwelekeo wa kidini na maadili, kukataa vurugu na kutovumiliana, kukuza hisia kwa uaminifu na ushiriki, pamoja na kufanya semina za kielimu, kidini, kijamii na kisaikolojia, pamoja na michezo na shughuli za burudani kwa ushiriki wa walemavu.

Back to top button