Habari

Waziri wa Rasilimali za Maji wa Misri ajadiliana na Mawaziri wa Umwagiliaji na Uwekezaji nchini Sudan Kusini njia za kuimarisha ushirikiano wa pamoja katika nyanja zote

Ali Mahmoud

Dkt. Sewilam:

– Mahusiano ya Misri na Sudan Kusini ni ya kina na yenye muda mrefu katika ngazi zote.

– Ushirikiano katika uwanja wa rasilimali za maji na umwagiliaji waendelea kwa miaka mingi, na Misri ina nia ya kutoa msaada wa kiufundi wa aina zote kwa ndugu nchini Sudan Kusini.

– Miradi ya pamoja ya maendeleo katika uwanja wa rasilimali za maji inalenga kuwahudumia wananchi wa Sudan Kusini mwanzoni.

– Kutosheleza maji safi ya kunywa kupitia vituo vya maji ya kunywa chini ya ardhi na uvunaji wa maji ya mvua.

– Kazi za kusafisha njia za maji kutokana na magugu maji huchangia katika kuhudumia urambaji wa mto na kupunguza hatari za mafuriko.

– Uanzishaji wa vituo vya kupima viwango na tabia kukusanya data za kihaidrolojia zinazohitajika kwa ajili ya maandalizi ya tafiti za pamoja za utabiri wa mafuriko na onyo la mapema.

– Kujali kwa usaidizi wa kitaasisi wa Wizara ya Umwagiliaji ya Sudan Kusini kupitia utafiti wa uanzishwaji wa kituo cha utabiri wa mafuriko na onyo la mapema, na kutunza mafunzo na kujenga uwezo.

– Misri ina nia ya kuimarisha mahusiano ya ushirikiano wa kiuchumi na Sudan Kusini na kuhimiza uanzishaji wa miradi ya uwekezaji.

– Kuwahimiza wafanyabiashara wa Misri kuchangia katika kuendeleza mzunguko wa maendeleo na uchumi kufikia maendeleo endelevu.

Ndani ya mfumo wa ziara yake ya kisasa kwa nchi ndugu ya Sudan Kusini … Mheshimiwa Prof. Hani Sewilam, Waziri wa Rasilimali za Maji na Umwagiliaji, alikutana na Mheshimiwa Pal Mai Deng, Waziri wa Rasilimali za Maji na Umwagiliaji wa Jamhuri ya Sudan Kusini, kwa mahudhurio ya Mheshimiwa Balozi Moataz Mustafa Abdel Qader, Balozi wa Misri kwa Sudan Kusini na ujumbe rasmi aliofuatana na Mheshimiwa Waziri, ambapo walijadili masuala ya ushirikiano wa pamoja kati ya nchi hizo mbili katika uwanja wa rasilimali za maji na umwagiliaji.

Dkt. Sewilam alisema kuwa kikao cha mazungumzo mazito kinalenga kujadili maendeleo ya kazi katika miradi ya pamoja ya maendeleo katika uwanja wa rasilimali za maji, inayokuja, mwanzoni, kuwahudumia wananchi wa Sudan Kusini kupitia kuwapatia maji safi ya kunywa, kama vile miradi ya kuanzisha vituo vya maji ya kunywa chini ya ardhi, pamoja na miradi ya kuvuna maji ya mvua kufaidika kutoka kwao katika utoaji wa maji ya kunywa na malisho ya mifugo na ulinzi kutoka katika mafuriko, pamoja na kuanzisha vituo vya kupima viwango na vitendo jijini Bor, Mji mkuu wa jimbo la Jonglei, kukusanya data na taarifa za kihaidrolojia zinazohitajika kuandaa tafiti za pamoja zinazochangia utabiri wa mafuriko na onyo la mapema la hatari za mafuriko.

Dkt. Sewilam alisisitizia utunzaji wa Misri kwa kazi za kusafisha mapito ya maji kutoka katika magugu ya maji, yanayochangia huduma ya urambazaji wa mto na kupunguza hatari za mafuriko na hivyo kufikia utulivu kwa wananchi, pamoja na utunzaji wa Misri kwa msaada wa kitaasisi kwa Wizara ya Rasilimali za Maji na Umwagiliaji nchini Sudan Kusini kupitia utafiti wa uanzishwaji wa kituo cha utabiri wa mafuriko na onyo la mapema, kama vile utunzaji wa mafunzo na kujenga uwezo.

Mheshimiwa, alieleza kuwa mahusiano ya Misri na Sudan Kusini ni ya kina na yanayoenea katika ngazi zote, haswa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika uwanja wa rasilimali za maji na umwagiliaji, ambao unaendelea kwa miaka mingi, na kwamba Misri ina uangalifu wa kutoa aina zote za msaada wa kiufundi kwa ndugu nchini Sudan Kusini.

Dkt. Sewilam pia alikutana na Mheshimiwa Dou Matouk, Waziri wa Uwekezaji nchini Sudan Kusini, ambapo walijadili nyanja za ushirikiano wa nchi hizo mbili na nafasi mbalimbali za uwekezaji katika nyanja zote kwa njia ambayo inafikia maslahi ya nchi hizo mbili na inaonesha vizuri wananchi wa Sudan Kusini.

Dkt. Sewilam a wakati wa mkutano huo, alisisitiza kuwa Misri ina uangalifu wa kuimarisha mahusiano ya ushirikiano wa kiuchumi na nchi ya Sudan Kusini, kuhimiza uanzishaji wa miradi ya uwekezaji na kuhimiza wafanyabiashara wa Misri kuchangia katika mzunguko wa maendeleo na uchumi wa Sudan Kusini kwa njia inayochangia kufikia maendeleo endelevu na kuinua kiwango cha maisha ya wananchi nchini Sudan Kusini.

زر الذهاب إلى الأعلى