Uchumi
Balozi wa Misri nchini Senegal akagua Mashamba Mawili ya Majaribio ya Mbegu za Ngano za Misri
Mervet Sakr
Kwa mwaliko wa Waziri wa Kilimo wa Senegal Ali Ngouille NDIAYE, Balozi Khaled Aref akiwa ameambatana na naibu wake, Katibu wa Tatu Amer Mazrou, alitembelea mashamba mawili kujionea matokeo ya kilimo cha majaribio cha mbegu za ngano za Misri za aina ya Beni Suef, Misri 1 na Misri 2, zilizoboreshwa katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo nchini Misri, katika maeneo ya Sangalkam na Beut.
Waziri huyo wa Senegal alipongeza uzalishaji wa mbegu za Misri, zilizopata matokeo yaliyozidi matarajio yao, kwani waliweza kukabiliana na mazingira na hali ya hewa nchini Senegal.