RAIS DK.MWINYI AISHUKURU KAMATI YA MWAKA MPYA WA KIISLAMU
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi amewashukuru kamati, viongozi wote wa dini pamoja na wadhamini waliochangia kufanikisha maadhimisho ya mwaka mpya wa Kiislamu.
Rais Dk.Mwinyi ametoa shukrani hizo leo Ikulu Zanzibar alipokutana na kamati ya maandalizi ya maadhimisho ya mwaka mpya wa Kiislamu yaliyofanyika mwaka huu Kisiwani Pemba, kwa nia ya kuwashukuru na tukio la ugawaji wa vyeti vya shukrani kwa kamati hiyo.
Naye, Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Saleh Omar Kaabi amemshukuru Rais Dk.Mwinyi kwa mwitikio wake na ushirikiano anautoa kwa Ofisi ya Mufti na kushiriki vyema kwenye mambo yenye heri.
Aidha, Rais Dk.Mwinyi amesema Serikali ilipokea kwa uzito mkubwa ombi la kamati hiyo la siku ya mapumziko ya kitaifa kila ifikapo maadhimisho ya mwaka huo na kueleza shukrani zakw kwa kamati hiyo kwa kuja na hoja hiyo ambayo ilikuwa na mafanikio makubwa.