Habari

RAIS DK.MWINYI AAGANA NA BALOZI WA INDIA TANZANIA

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amekutana na Balozi wa India nchini Tanzania, Mhe.Binaya Srikanta Pradhan  Ikulu Zanzibar kumuaga baada ya kumaliza kipindi cha miaka mitatu ya utumishi nchini tarehe: 22 Desemba 2023.

Rais Dk.Mwinyi amemshukuru kwa niaba ya Serikali ya India kwa kudumisha ushirikiano na uhusiano wa kidiplomasia katika kipindi chake cha uwakilishi ikiwemo upatikanaji wa fursa mbalimbali za ufadhili wa masomo India, kuanzishwa kwa Taasisi ya IIT Madras Zanzibar, miradi mbalimbali ya maendeleo, kujenga uwezo , pamoja na fursa za uwekezaji na biashara.

Naye , Balozi Mhe.Binaya Srikanta Pradhan  amezungumzia kuhusu Serikali ya India kuwapeleka kikundi cha Zanzibar One Modern Taarab kutoka Zanzibar kushiriki Tamasha la Utamaduni nchini India mwezi Februari mwaka 2024.

Pia Balozi Mhe.Pradhan amemwalika Rais Dk.Mwinyi kuitembelea India, Rais Dk.Mwinyi amekubali mwaliko huo wa kuitembelea India.

زر الذهاب إلى الأعلى