Habari Tofauti

Mwenyekiti wa Mamlaka ya Dawa ashiriki katika toleo la kwanza la Jukwaa la Soko la Wazalishaji wa Afrika katika Ufalme wa Morocco

0:00

Dkt. Tamer Essam, Mwenyekiti wa Mamlaka ya Misri ya Dawa , alishiriki katika toleo la kwanza la Jukwaa la Soko la Wazalishaji wa Afrika lililofanyika Morocco, ambapo alishiriki wakati wa vikao vya jukwaa, na kuwasilisha maoni ya Mamlaka na huduma zinazotolewa katika uwanja wa kuimarisha sekta ya chanjo nchini Misri, haswa kuhusiana na Mamlaka ya Dawa ya Misri kupata kibali cha Shirika la Afya Duniani katika uwanja wa chanjo.

Wakati wa mkutano huo, uwezo wa utengenezaji na mipango ya sasa ya upanuzi katika viwanda vya ndani na vya kikanda, haswa tasnia ya chanjo Barani Afrika, ilipitishwa.

Mkutano huo ni wa kwanza wa Baraza Kazi la Mawaziri katika ngazi ya Bara la Afrika, ambao una jukumu la kujifunza uanzishaji wa jukwaa la utengenezaji wa dawa Barani Afrika, haswa utengenezaji wa chanjo, unaolenga kufikia uzalishaji wa asilimia 40 ya mahitaji ya Bara la Afrika ya chanjo ifikapo mwaka 2040, pamoja na maendeleo ya utaratibu wa ununuzi wa pamoja kwa Bara la Afrika wa maandalizi ya matibabu, hasa chanjo ili kuhakikisha umoja wa viwango vya ubora, ufanisi na usalama.

Ushiriki wa Mamlaka ya Dawa unakuja kwa kuzingatia nia yake ya kuimarisha uhusiano na kuongeza matarajio ya ushirikiano na nchi za Kiarabu na Afrika, pamoja na nia yake ya kushiriki uzoefu wake katika uwanja wa ujanibishaji na utengenezaji wa chanjo za kimkakati.

Back to top button