Habari Tofauti

RAIS DK.MWINYI AZITAKA TAASISI ZA SERIKALI KUONDOA URASIMU KATIKA BIASHARA NCHINI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amezitaka taasisi zinazosimamia biashara kuhakikisha zinaondoa urasimu na kuwawezesha wafanyabiashara  nchini kwa kuwekea mazingira rafiki ya biashara zao.

Ameyasema hayo  wakati akifunga Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam katika ukumbi wa Rashid Mfaume Kawawa, uwanja wa Maonesho wa Mwalimu Julius Nyerere  Jijini Dar es Salaam leo tarehe 13 Julai 2023.

Aidha , Rais Dk.Mwinyi amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zitashirikiana  katika kuhamasisha ukuaji wa biashara na uwekezaji kwa kufanyia kazi maoni ya wafanyabiashara nchini.

Pia kwa kuboresha mazingira ya biashara  kwa kuwezesha taasisi  za Serikali kuwa na mifumo inayosomana itakayoweza kupunguza gharama zisizo za lazima na kuondoa utitiri wa tozo katika biashara nchini.

Maonesho hayo ya 47  kwa mwaka huu  yameshirikisha jumla la kampuni 3500, kampuni  267 ni kampuni za nje ya Nchi kutoka Nchi 17 na kutembelewa na wananchi takribani Milioni 3.

زر الذهاب إلى الأعلى